Muhraja's après ski & nocturnal English language course
Tenses (nyakati) Home
Tenses ni maneno yanayoonyesha hali ya kitendo ya wakati wake uliofanyika, mathalan, katika Kiswahili, mtu akisema, alikwenda, anakwenda, atakwenda. Hayo yote ni maneno yenye maana moja. Lakini tofauti yake ni hali ya wakati wa kufanyika kwa tendo hilo.
Katika lugha ya Kiswahili, inasemekana kuwa kuna tenses (nyakati) tatu, nazo ni
Wakati uliopo (simple present tense)
Wakati uliopita (simple past) na
Wakati ujao (simple future)
Vivyo hivyo ndivyo Kiingreza kilivyo, nacho kina tense za namna hiyo hiyo,ingawa kimuundo na matumizi haziwezi kuwa sawa, tunajua kuwa kuna hali za tenses hizi, mfano,
Hali ya kukamilika (perfect tense), mfano: nimekula, kitendo cha kula kinaonyesha ukamilifu wake, yaani kimetimia au kimeacha athari hadi sasa hivi. (yaani kwa ujumla kitendo hicho kina uhusiano mkubwa na wakati uliopo ingawa kimepita
Hali ya kuendelea (progressive tense), mfano:ninakula, kitendo cha kula kinaonyesha kuwa bado kinaendelea wakati huu huu tunaozungumzia na bado hakijamalizika.
Wakati uliopita hali kamilifu inayoendelea/ijayo/iliyopita (Present perfect progressive/ future/past/) n.k
Kumbuka kuwa, katika Lugha ya Kiingereza, mambo hayo yote yapo; kama unahitaji kujua somo miongoni mwa hayo, click katika mada inayohusika hapo chini;
Katika mpangilio mzuri wa maelezo ya tenses hizi ni kama ilivyoonyeshwa hapo chini
Present
Past
Future
Maneno mengine ambayo yanaweza kutumiwa katika tenses ni kama utakavyoyaona wakati utakapokuwa unaendelea kusoma tenses;
Zingatia; Kila tense ina matumizi yake, hazilingani kwa matumizi tense moja na nyingine, Kuwa mwangalifu! Dhumuni la kukuletea somo hili ni kuwa uweze kutofautisha na ujue matumizi ya kila moja hapo utakapofikia mwisho wa somo lako hili.
nakutakia kila la kheri katika usomaji wako;
By Muhseen bin Rajab (Canoksan)
Wednesday, August 21, 2002