TENSES
PAST PERFECT PROGRESSIVE (wakati uliopita hali timilifu inayoendelea)
Past perfect progressive (continuous)
Itakumbukwa
kuwa,kila lugha ina tenses (nyakati ambazo zinaelezwa na verbs za lugha husika)
sio kila tense tutakayokuwa tukieleza hapa kwa kuitolea mifano ya kuifananishia
na tenses itakuwa na sifa sawa na ya Lugha ya Kiingereza
Past
perfect continuous imejengwa na maneno mawili -past perfect ya verb to be (Na
hii ni neno "had been") ikifuatiwa na
present
participle ya verb husika (Yaani Verb+ing). Tunapoongelea verb husika
ni kuwa, tunaongelea kuhusu kitendo kilichomuelekea
(Subject) yaani mtajwa/
mtendaji katika sentensi hiyo
Mifano:
Subject | had been | verb-ing |
I
He They You We She Abdur Rauuf |
had
been
had been had been had been had been had been had been |
writing
talking speaking ignoring studying cooking typing |
Affirmative | had been | verb = ing |
She You They We I |
had been had been had been had been had been |
driving surfing smoking cleaning bathing |
Negative | had been | verb + ing |
We I They You Ali Hilal AbdulQaadir |
hadn't been hadn't been hadn't been hadn't been hadn't been hadn't been hadn't been |
sleeping nodding off writing drawing mopping peeling watching |
Interrogative | ||
Had you Had you Had he Had she Had they |
been been been been been |
eating? singing? eating? witting? learning? |
Interrogative negative | ||
Hadn't they Hadn't he Hadn't dog Hadn't the pupils Hadn't you |
been been been been been |
swimming? persecuting? barking? sweeping blaming? |
Mfano: neno kucheza (play) katika hali zote tatu tulizosoma hapo juu
Affirmative |
Negative |
Interrogative |
I had been playing |
I hadn't been playing |
Had I been playing? |
You had been playing |
You hadn't been playing |
Had you been playing |
He had been playing |
He hadn't been playing |
Had she been playing? |
We had been playing | We hadn't been playing | Had we been playing? |
You had been playing | You hadn't been playing | Had you been playing? |
They had been playing | They hadn't been playing | Had they been playing? |
She had been playing | She hadn't been playing | Had she been playing? |
It had been playing | It hadn't been playing | Had it been playing? |
Hilal had been playing | Hilal hadn't been playing | Had Hilal been playing? |
Matumizi yake: Kumbuka kuwa, tense hii haitumiki kwa verbs ambazo haziko kwenye progressive form (yaani hazina kuongezewa mwishoni ..ing) ila maneno kama "want' na wakati mwingine "wish"
mfano; She had been wanting to to purchase a new car for a long time. na kitu kingine cha kukumbuka ni kuwa, tense hii haina passive form (kutendewa)
Kazi ya past perfect progressive (past perfect continue) tense
1.
Past perfect continuous huafikiana na present perfect progressive, lakini
katika kurejea wakati huko nyuma kidogo kuliko, yaani wakati kabla ya sasa. Pia,
hutumika pale tunapokuwa na shauku ya kujua kuhusu wakati huo ulivyokuwa unaendelea.
Je, umekuwa ukinisubiri kitambo kabla ya simu kuita? hapa Msemaji ana shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea katika wakati huo uliopita kidogo kabla ya wakati huo anapoongelea. Tazama mifano zaidi,
a. Had
you been waiting long before the telephone call?
b. They had been having
lunch before the guest arrival.
c. His head had been aching severely
for several hours before he got sleep.
d. Their friends had been trying
to rescue them when the building that they were inside got crashed.
Hali hii hutumika vile vile katika reported speech. Ni sawa na ile ya past progressive na present perfect progressive katika direct speech:
Abdul Maalik said "I have been surfing wind all afternoon." Abdul Maalik said he had been surfing wind all afternoon.
When Hilal asked by a judge whether he was by the time his computer stolen, he said "I was reading newspaper in my bedroom." When the police questioned him, John told them he had been reading news paper in his bedroom.
2. Past perfect progressive huwa ina uhusiano wa aina moja na past perfect ikiwa present perfect progressive huwa kwenye present perfect, Ikiwa kitendo kilianza kabla ya kuongea katika wakati uliopita na kikaendelea hadi muda huo au kikasimama au kikakoma au kikaisha kabla, twaweza mara nyingi kutumia kati ya tense hizi mbili,
It was now eleven and he got tired because he had worked since dusk = hii ni sawa na kusema
It was now eleven and he got tired because he had been working since dusk.
Mfano mwingine ni kama;
They were having their lunch when I arrived here (But they've just finished off) =
They had been having their lunch when I arrived.
Sentensi hizo hapo zinamaanisha kuwa mtu huyo aliyetajwa kuhusika na kufanya kitendo alikuwa katika kuendelea kufanya kitendo hicho ambacho kilianza kabla ya mzungumzaji kukizungumzia na kuendelea hadi hapo muongeaji alipokuwa akiendelea au kilikuwa ndio kimesimama sio muda mrefu, yaani ndio sasa hivi tu kimesimama na hakiendelei tena.
Kwa maelezo zaidi ya matumizi ya tense hii, click hapa
Passive form
Tense hii haina passive form
Msamiati
Kabla sijafunga somo langu nitakupa maana ya maneno baadhi niliyoyatumia humu
Dusk = alfajiri, wakati kabla ya asubuhi (kama saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili hivi)
get tired (=Be tired) = choka, Wind surfing = punga upepo, ignore = puuza, bathing = oga
Persecute = tesa mtu kwa sababu ya dini yake, ache = uma, maumivu (mfano, headache = maumivu ya kichwa)
blame = laumu
Nakutakia kila la kheri na ninakukaribisha uendelee na masomo mengine.