![canoksanhilal swahili English page](present_progressive_tense_files/image001.gif)
PRESENT PROGRESSIVE TENSE. (Wakati uliopo hali inayoendelea)
Hali yake (Kanuni) ya muundo
Present
progressive ya verb yoyote imejengwa na sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni
present tense ya verb "To be" + present participle ya kitenzi kikuu
(main verb.)
Yabidi
tukumbuke kuwa tuna present mbili katika Kiingereza, nazo ni
-Present progressive
tense (Wakati uliopo hali ya kuendelea), mfano : I am walking
-Simple
Present (wakati uliopo); I walk.
(Hali au muundo wa
present participle ni: base+ing, mfano; walking, playing, moving, smiling)
Affirmative
(Maelezo) |
Subject |
+ to be
|
+ base+ing
|
she |
is |
walking
|
|
|
|
Negative
(Makanusho) |
Subject |
+ to be + not
|
+ base+ing
|
she |
is not (isn't)
|
walking
|
|
|
|
Interrogative (Maulizo) |
to be |
+ subject |
+ base+ing
|
is |
she |
walking?
|
Mfano: "Kwenda" ( to
go,) present progressive.
Affirmative (Maelezo) |
Negative (Makanusho) |
Interrogative (Maulizo) |
I am going
|
I am not going
|
Am I going?
|
You are going
|
You aren't going.
|
Are you going?
|
He, she, it is
going |
He, she, it isn't
going |
Is he, she, it going?
|
We are going
|
We aren't going
|
Are we going?
|
You are going
|
You aren't going
|
Are you going?
|
They are going
|
They aren't going
|
Are they going?
|
Kumbuka:
mara nyingi hufupishwa verb "to be" na kufupishwa kama hivi; badala ya I am
huwa I'm, You are (You're) He is (He's) We are (We're) They are (They're) n.k.na
kuwa kama hivi
I'm seeing Hilal
tomorrow.
You're having
meeting tonight.
They're trying to
solve it.
2.
Present progressive, Kazi zake.
Kama ilivyo
katika tenses zote za Kiingereza tunazojua, malengo/mwelekeo wa mzungumzaji ni
wa muhimu kwa wakati wa wakati wa kitendo au tukio.
Wakati mtu anapotumia present progressive tense huwa anafikiria kuhusu kitu
ambacho hakijakamilika na hakijaisha bado.
The present progressive
hutumika:
- Kuelezea kitendo
ambacho kinaendelea hadi wakati huu tulionao. mfano.
You are watching
the football match. We are studying
English grammar.
- Kuelezea kitendo
ambacho kinaendelea katika kipindi hiki au mwenendo. mfano; Are you still working for the same
company? More and more people are becoming
vegetarian.
- Kuelezea kitendo au
tukio katika wakati ujao ambalo/ambacho kimeshaandaliwa au kupangwa tayari kwa
kufanywa (kuandaliwa) mfano; We're having
meeting tonight. We're going
on holiday tomorrow. I'm meeting my
boyfriend tonight. Are they visiting
you next winter?
- Kuelezea tukio
lisiloendelea moja kwa moja au hali, mfano; He usually plays the drums, but
he's playing bass guitar tonight.
The weather forecast was good, but it's raining
at the moment.
- Zikiwa na maneno kama 'always, forever,
constantly', hutumika kuelezea na kuhimizia kwa msisitizo mfululizo
unaoendelea wa vitendo vinavyojirudia rudia, Mfano. Harry and Sally are always arguing!
You're forever complaining about your
mother-in-law!
Angalia!
Baadhi ya verbs (Vitendo)
hazitumiwi katika hali ya kuendelea (Progressive form, angalia hapo chini)
3.
Verbs ambazo kwa kawaida hazitumiki katika progressive form
(muundo wa kuendelea)
Verbs
zilizoorodheshwa hapo chini kwa kawaida hutumika katika muundo wa simple kwa
kuwa huzirejea hali kuliko vitendo au harakati:
List of common verbs
normally used in simple form:
Hisia/maono/utambuzi |
feel*,
hear, see*, smell, taste
|
Maoni |
assume, believe, consider, doubt,
feel (= think), find (= consider), suppose, think*
|
Hali za kiakili/kifikra |
forget, imagine, know, mean,
notice, recognize, remember, understand |
Hisia/tamaa |
envy, fear, dislike, hate, hope,
like, love, mind, prefer, regret, want, wish
|
Vipimo |
contain, cost, hold, measure, weigh
|
mengineyo |
look (=Fanana), seem, be (katika
mahali pengi hutumika), have (wakati ikiwa inamilikiwa)*
|
Zingatia:
1. Vitendo vya verbs (see, hear, feel,
taste, smell) mara nyingi hutumika na neno"can" mfano: I can see..
2.
*
Verbs hizi huweza kutumika katika muundo wa kuendelea, lakini kwa maana
tofauti. Fananisha;
a.
This coat feels nice and warm. (= Utambuzi
wako juu ya sifa za koti.)
b.
John's feeling much better now (= Afya yake inaendelea kuwa nzuri)
a.
She has three dogs and a
cat. (=Umilikaji)
b.
She's having supper. (= anakula sasa hivi.)
a.
I can see Anthony in the
garden (= maono)
b.
I'm seeing Anthony later (= tumepanga
kuonana na Anthony)
Mifano:
- I
wish I was in Germany now.
- She
wants to see him now.
- I don't
understand why he is shouting.
- I
feel we are making a mistake.
- This glass
holds half a liter.
Kazi za tense hii kwa muhtasar.
1. Hutumika kuelezea vitendo vinavyofanyika sasa hivi.
Mfano;
It is raining.
The wind is blowing.
2. Kwa kitendo kinachofanyika katika kipindi hiki lakini sio lazima katika
wakati wa kuzungumza, Mfano
He is teaching English and learning Computer
technology. (anaweza akawa hafanyi hata kimoja katika hivyo katika wakati huo
wa kuongea)
I am playing football (Hii yaweza kuwa
inafanyika katika kipindi cha kuongea, lakini sio yaweza pia kuwa na maana ya
"sasa" kwa maana ya ujumla.
Kumbuka kuwa, wakati present progressive ikiwa na
subject moja (Mtendaji mmoja wa kitendo), matendo yake yataunganishwa na
kiunganishi "And" . tazama mfano hapo chini;
I was cooking and washing my utensils.
3. Hutumika katika mipangilio yenye maalum katika wakati ujao wa karibu (Njia
ambayo ni ya kawaida sana ya mtu kueleza mipangilio yake ijayo
punde). hii hutumika pale maandalizi yameshakamilika kufanyika, mfano;
I'm meeting Hilal tonight. He is taking me to Abdul's home.
Are you doing anything tomorrow morning?
Yes. I am visiting my aunt at Ukonga.
Zaidi kuhusu matumizi ya tense hii
click
hapa
Tunapoongelea kitendo ambacho kinaendelea tu kufanyika wakati huo huo wa
kukiongelea, tunatumia tense hii, Hii ina maana kuwa, ukiwa sasa hivi unaandika,
na mtu anakuuliza kuwa unafanya nini (sasa hivi), utamjibu kwa kusema "ninaandika..."
Kwa maana hiyo basi, tunaona kuwa neno lililokolezwa hapo ni "..na.."
kutoka kwenye maneno "ninakula,
tunakula, wanakula,
anacheza n.k
Katika lugha ya Kiingereza tunatumia auxiliary verbs (vitenzi visaidizi/
neno linalosaidia kitendo kikuu) ambalo katika tense hii ni verb "to be" (yaani
am,
are na
is") kutegemeana na
subject
uliyotumia.
I am + present
participle ya verb husika. yaani itakuwa hivi (I am ikifuatiwa na neno lenye
kuishia na ...ing)
I am writing it.
You are playing
They are dancing.
You are blaming him.
They are trying to cheat us.
She is solving the problem.
Hilal is talking with his teacher.
We are surfing the website.
He is doing his work with perfect aplomb.
Tukiwa tunahitaji kuuliza maswali juu ya mambo
fulani, katika lugha ya Kiingereza mara nyingi mwanzo wa sentensi ya Maswali
tunaanza kwa
auxiliary verb
ya tense hiyo kutegemeana na subject tunayoitumia.
Kwa mfano, katika sentensi ya startment (maelezo)
kama ilivyo hapo juu kwenye sentensi tulizokwisha taja, utakuta kuwa, baada ya
subject kinachofuatia ni
auxiliary verb na
kuishia na main verb.
katika sentensi ya maswali (interrogative sentence) inakuwa kama hivi:
auxiliary verb
+ subject +
verb (in present perfect
form) nayo ni kama hivi:
Are you eating?
Are they coming?
Are we reading?
Am I writing?
Are you playing?
Are they dancing?
Are you blaming him?
Are you trying to cheat us?
Is she solving the problem?
Is Hilal talking to his teacher?
Are we surfing the website?
Is he doing his work with perfect aplomb?
Tukiwa tunahitaji kuziandika katika tags questions sentensi za namna hii
inabidi tuanze na verb "to be" kisha kuandika kinyume nyume, yaani kama sentensi
i katika
affirmative form iwe katika
negative form.
Mfano; maana.
You are walking, aren't you? wewe unatembea. au
siyo?
They are driving, aren't they?
We are surfing the web, aren't we?
He is playing football, isn't she?
Angalia hizi hapa chini za negative,
She is not driving, is she?
They are not talking, are they?
He is not playing, is he?
We are not surfing a web, are we?
maneno yaliyo tumika hapo juu na maana zake.
Verb to infinitive without "to"
present participle. maana
write
writing Andika.
Play
playing cheza.
dance
dancing. cheza (musiki au nyimbo yoyote.)
Blame
blaming laumu.
try
trying jaribu.
solve
solving tatua.
talk
talking kuzungumza.
surf (web)
surfing kutembealea website
do
doing kufanya kitu.
Cheat
cheating kudanganya.
mengineyo ni kama:
Aplomb _ kufanya kitu kwa usahihi bila mashaka, kwa kujiamini. mfano
He is doing his homework with perfect aplomb
_ yeye anafanya kazi yake ya nyumbani kwa ukamilifu wa kujiamini
Problem = tatizo, swali linalohitaji kutafutiwa ufumbuzi.
Ninakutakia kila la kheri katika kuendelea na masomo yako;
Ikiwa una swali lolote juu ya mada tunazozitoa humu na masomo kama hujaelewa
vizuri au unahitaji kuchangia kuelewesha wenzako, usisite kuwasiliana na sisi
katika e mail address hii
Canoksan@yahoo.com au
hilalshukri@yahoo.com
|