Dictionary  home Qur'aan Islamic studies  home English main page sentences pattern 

Muhraja's après ski and nocturnal English program center - Sentence patterns

Sentence patterns

  Tunapozungumzia kuhusu somo hili tunaelezea au kufafanua kuhusu miundo ya sentensi, 

   Hebu tuzigawanye hizi katika makundi ili tuone namna hizi patterns zinavyokuwa katika sentensi. 

  Sentence pattern one

  Angalia sentensi ifuatayo:

     Hilal, who was standing at the door, laughed heartily as the boy fell off his bike.

   (Hilal, ambaye alikuwa amesimama kwenye mlango, alicheka kimoyomoyo alipoanguka mvulana huyo kutoka juu ya baiskeli yake)

   Katika sentensi hiyo hapo juu kuna maneno mawili ambayo yameandikwa kwa italic, maneno hayo ni Hilal, ambalo ni subject na ni jina noun na neno laughed ambalo ni verb. Haya maneno mawili Haya maneno mawili hutengeneza msingi wa sehemu ya sentensi nzima. Maneno mengine yote yaliyobakia ni kama yanasaidia tu kutoa maana zaidi ya sentensi pattern, na hutoa maana pana zaidi.

        Hapa tutaita "Hilal laughed" (Yaani katika ile tafsiri ya sentensi kwa Kiswahili tungesema "Hilal alicheka") Fananisha sentensi hapo juu na uangalie muundo wake, kisha uangalie hiyo hapo chini ili ujuie kwa nini tunasema kuwa maneno mawili yaliyopigiwa mstari ni maneno ya msingi katika kila sehemu ya sentensi na yale yaliyobakia katika senternsi ya juu yanatumika katika kuelezea tu maana pana zaidi ya sentensi.

          Kumbuka kuwa hii pattern, twaweza pia kutumia pronoun katika sehemu ya noun. Tutaona kuwa tunaweza kutumia pronoun inayofaa wakati wowote iwapo noun hutokea ndani ya sentence pattern yoyote ambazo tutazisoma humu Inshaallah. Hapa tuone mifano michache ya sentence pattern One:

      Birds flew.            Student learns           we eat                            I teach

      Fire burns.            Cars roars.               They like us.                   Girl smiled.

  Katika sentensi zote hapo juu, tunaweza kuona kuwa zimebeba maneno mawili muhimu, yaani nouns au pronouns na verbs. Mara nyingi hatutumii sentensi ambazo ni nyepesi zenye maneno machache kama hizi katika lugha ya Kiingereza. Vyote nouns na verbs kwa kawaida huelezewa katika njia moja au zaidi kama ilivyooneshwa katika sentensi ya mwanzo hapo tulipokuwa tukilianza somo letu. vile vile mifano zaidi tutaona mbeleni Inshaallah.

   Vile vile kumbuka kuwa hatungetakiwa kuchukua mfano wa sentensi pattern One ambayo tumeiona mwanzoni mwa somo kama mfano na tukazifanya sentensi nyingine zote za pattern hii kuwa zitachukuliwa kama ni sahihi na kamili kama yenyewe ilivyo, mfano tukasema "Hilal laughed." Hii haitakuwa kwa kawaida. ikiwa tutachukua maneno mawili hayo kutoka katika sentensi pattern One , moja katika mifano miwili ya sentensi pattern One kama ifuatavyo hapa chini; (haya maneno mawili yapo katika italic) utakuwa kwa hakika umepotea na utakuwa umetengeneza sentensi ambayo sio sahihi hata kidogo Kisarufi, ila tu utakuwa umetengeneza sentensi kama mfano sahihi wa sentence pattern One,

The doctor told the patients to stay in his bed room.

They began with a high life.

      Hili litazihusu sentence patterns zote tutakazokuwa tukizielezea.

Makosa ya kuyaepuka katika sentences patterns;

    Inabidi tudhihirishe wazi hapa kuwa Kila wakati wewe ni lazima kuwa muangalifu kuwa utengeneze sentensi pattern kiusahihi. Mfano; "Cars roars" au "He laugh" ni makosa. Hili laweza kuwa wazi, lakini wakati subject na verbs ya sentensi pattern ikiwa imetenganishwa kwa maneno mbalimbali mengine, kosa la namna hii hutokea mara nyingi. Jihadhari! Chukua mifano hii ifuatayo;

        The boys in the top class leave rather later than the others.

    Sehemu za msingi katika sentence hii ni "Boys leave'. haitakiwi kuwa "Class leave" Hii itakuwa sio sahihi, tunaweza kuona wazi kuwa katika mfano huo hapo juu, mtu angeweza kusema

            "The boys in the top class leaves rather later than the others" Sentensi hii sio sahihi hata kidogo.  

   Hili ni kosa ambalo ni lazima uwe muangalifu uliepuke, sio tu katika sentence pattern One, lakini pia katika sentence patterns zote utakazosoma. 

 Prepared by Muhseen bin Rajab (Canoksan)

Sunday, August 04, 2002