.
(SOME OF VEGETABLE & SPICES' NAME) (BAADHI YA MAJINA YA VIUNGO NA MBOGA MBOGA)
Unaweza kuclick kwenye jina la kiungo au mbogamboga ili ukione kwa picha, hii itakurahisishia kazi ili uelewe ni kiungo au mboga gani yenye jina ulilo lisoma; natumaini utaniandikia ikiwa unajua kwa Kiswahili majina ambayo sijayataja katika Kiswahili,
Anuani yangu ni canoksan@yahoo.com au hilalshukri@yahoo.com , nategemea kupokea kutoka kwako. nakutakia masomo mema.
A tomato nyanya.
Cinnamon mdalasini.
Averrhoa bilibi mbilimbi.
A brinjal bilinganya.
An aubergine bilinganya.
A coconut nazi.
A ginger tangawizi.
Cooking oil mafuta ya kupikia.
Paprika pilipili hoho.
Leek aina fulani ya kitunguu kidogo.
Greens mboga za majani.
carrot karoti.
Cardamom iliki.
Capsicum Pilipili hoho.
Curry powder mchanganyiko wa viungo vilivyosagwa kama vile mdalasini, iliki n.k
Lettuce mboga ya majani ya kizungu, saladi.
Coriander giligilani
Turmeric manjano
Citronella mchaichai.
cumin jamda, jira, kisibiti.
Mushroom uyoga.
Almond Kwa Kiarabu ni 'lawz' na kwa Kiswahili ni lozi.
Sesame ufuta. na (Kwa kiarabu huitwa 'sasim' au 'zilzlani'
Chile Tazama 'capsicum' hapo juu.
Tamarind ukwaju.
Vanilla lavani.
Assafoetida Kwa Kiingereza huitwa sticking gum au devil dung, kwa Kiswahili ni 'mvuje'
All spice kwa kiarabu huitwa bahar, bar hub wa nai'm.
Fennel seeds mbegu za shamari.
Capers mruko, mchezo.
Coffee kahawa.
Fennel shamari.
Safflower kwa kiarabu linaitwa 'usfur'
Galangale hili hujulikana kwa Kiarabu kama "adkham"
Lemon limau.
Saffron kwa kiarabu huitwa za'fran, vile vile kwa Kiswahili huitwa zafarani, Kiswedish ni safran na Spanish ni azafa'ni.
Salt Chumvi.
Sesame seeds mbegu za ufuta.
Tea chai
Ajwain (kwa kiarabu huitwa 'buranikataya' au 'Twalib el kuubs'
Black mustard hardali.
Fenugreek uwatu, (na kwa lugha ya kiarabu huitwa 'hulba'
Bitter almond Lozi chungu, (lawz murr)
Licorice kwa neno lingine hujulikana kwa Kiingereza kama liquored, hili huitwa kwa Kiarabu "arqsus"
ambapo kwa Kiswahili huitwa "susu" na neno hili la Kiswahili limetokana kwenye Kiarabu.
Nigella Kwa Kiarabu huitwa "Habbat sawda" au "habbat baraka" ambapo kwa Kiswahili ni habat soda.
N.B Katika kutumia kwangu baadhi ya majina ya Kiarabu ni kuwa, (i) Kiswahili kimejengwa kwa kiasi kikubwa kutokana na maneno mengi ya Lugha ya kiarabu
(ii) Katika viungo vingi ambavyo vingine hutumika kama madawa, vimekuwa vikiuzwa na Waarabu hapa afrika
mashariki na hata yamekuwa yakitumika majina ya viungo hivyo kwa Kiarabu,
Kutokana na sababu hizo mbili zenye uzito hapo juu, ni njia rahisi kwa mfuatiliaji kuelewa na hata kuweza kuviona au
pale anapoviona avitambue.
Natumaini mtaniandikia ili mnieleweshe pale ambapo mnafahamu majina halisi ya viungo ambavyo sikuweza kuviandika humu kutokana na kutojua vinaitwaje kwa Kiswahili wala kwa kiarabu.
Kutumika maneno ya lugha mbalimbali katika kukopeshwa kwenye lugha nyingine ni kitu cha kawaida sana, hapa nitakuonyesha mfano kuwa, hata baadhi ya maneno ya Kiarabu yametumika katika Kiingereza, mfano hapo juu neno
"tamarind" limetokana na neno la Kiarabu ambalo kiungo hiki kinaitwa "tamr hindi " neno tamr kwa kiarabu ni tende
na Hindiy' ni ya Kihindi kwa maana hiyo neno hilo tamr hind lina maana ya tende ya Kihindi, hii ni kutokana na kuota sana kwa wingi huko India. hii ndio sababu Waarabu wameiita "tende ya kihindi" neno hili tamr hind ndio likachukuliwa kwenye Kiingreza na kuitwa "tamarind".
Ninakutakia kila la kheri katika kuendelea kutafuta masomo zaidi humu.