![]() |
Tell me when this page is updated |
Muhraja's aprč³ ski & nocturnal English language program
BAADHI YA MAJINA YA WANYAMA WA NYUMBANI KWA KIINGEREZA.
(SOME OF LIVE STOCK NAMES )
<
A goat mbuzi.
A dog mbwa.
A pig nguruwe.
A hen kuku.
A duck bata.
A donkey punda.
A guinea fowl kanga.
A camel ngamia.
A horse farasi.
A sheep kondoo.
A cat paka.
Puppy mwana mbwa,
A kitten mwana wa paka.
A chick mwana kuku.
A foal mwana farasi.
A duckling mwana wa bata.
A lamb mwana wa kondoo.
BAADHI YA MAJINA YA WANYAMA WA PORINI NA MAJINI
(SOME OF SEA AND WILD ANIMAL NAMES)
Vermin wanyama/wadudu waharibifu wa mali na kuleta hasara (mfano, panya, simba, kunguni n.k)
Prey wanyama/ndege/wadudu wawindwao kwa chakula mfano yule anayemuua mnyama
mwenzie au ndege mwenzie ili amle, yule aliyeua ni "prey" mfano tai, lion n.k.
Beast mnyama yeyote aliye na miguu minne huitwa "beast" (Kwa ujumla)
Biped mnyama yeyoye mwenye miguu miwili tu huitwa "Biped"
Amphibians mnyama yeyote awezaye kuishi majini na nchi kavu: mathalan Chura n.k
A bear dubu.
An ass mnyama jamii ya farasi mwenye masikio marefu na mwishoni
mwa mkiawe analo fungula manyoya mwishoni mwa
mkia (turft) kama alivyo nalo ng'ombe.
An elephant tembo.
An ostrich mbuni.
A lion simba.
A zebra pundamilia.
A rhino kifaru.
A giraffe twiga.
A crocodile mamba.
A squirrel kicheche.
A mongoose sili, nguchiro.
A leopard Chui.
A monkey kima.
A gorilla sokwe.
A hippopotamus kiboko.
A hyena fisi.
A chameleon kinyonga.
A lizard mjusi.
A buffalo nyati.
A fish samaki.
A snake nyoka.
A rat panya (wa nyumbani).
A flamingo aina ya ndege mwekundu mwenye miguu mirefu akaaye majini.
A hyrax wibari, kiwanga.
An ichneumon kinyama kidogo kama paka kiuwacho nyoka, nguchiro.
A jackdaw ndege mweusi kama kunguru vile alivyo halafu ni mwizi sana.
A jackal mbweha
A jay ndege mithili ya kunguru mdogo mwenye rangi nzuri na milio
mingi.
A king fisher mdiria, dete pwani.
A crane korongo
A lamprey aina ya samaki kama mkunga.
A lapwing aina ya ndege
A lemur kamba wa bukini.
A leveret mwana wa sungura, kisungura.
A fawn mtoto wa deer/ paa au kulungu mdogo).
A leviathan mnyama yeyote mkubwa aishiye baharini.
A limpet namna ya koa wa baharini anayeambatana sana na miamba.
A parrot kasuku.
A daw ndege kama kunguru mdogo.
An elk mnyama kama kulungu mkubwa mwenye pembe za panda panda.
A peacock tausi.
A lynx mnyama kama paka wa mwitu mwenye macho makali sana.
A magpie ndege kama kunguru.
A mallard bata mwitu.
A deer kulungu, mnyama mfano wa paa.
A dugong nguva.
A dolphin samaki anayefanana sana na nyangumi lakini yeye ni mdogo.
A martin ndege kama mbayuwayu.
Menagerie jamii ya wanyama wa mwitu watembeao katika vitundu ili watu
wawaone.
A mink mnyama mdogo mithli ya kicheche akaaye majini na nchi kavu mwenye ngozi iuzwayo kwa bei ghali.
Minnow samaki mdogo wa mtoni.
A mole mnyama mdogo mwenye rangi ya majivu afukuaye chini, fuko.
Mullet namna fulani ya samaki.
A mussel kome, kijogoo.
A narwhal namna ya nyangumi mdogo.
A turkey bata mzinga.
A falcon ndege jamii ya "prey.
An eagle tai.
A kiwi ndege John
An octopus pweza.
A dove/ pigeon njiwa
A hedgehog mnyama kama nungunungu mdogo.
A hawk kengewa, hajivale.
A hart mnyama kama paa dume, ayala.
A hartebeest kongoni.
A kite ( a bird of prey) mwewe
Antelope swala.
A hedge sparrow namna ya ndege mdogo.
A heifer mtamba wa ng'ombe, (mtarika wa ng'ombe), mori.
A grampus mnyama mkubwa wa baharini kama pomboo.
A haddock aina fulani ya samaki wa baharini.
A heron yangeyange.
Herrings aina fulani ya samaki wa baharini.
A fox mnyama mithili ya mbweha.
Gallinaceous jamii ya kuku, kanga n.k
A cormorant ndege wa bahari alaye samaki, mnandi.
A cobra aina ya nyoka anayevimbisha shingo yake, swila.
A cockatoo aina fulani ya kasuku.
A gnu nyumbu.
Baboon nyani mkubwa mwenye uso kama wa mbwa.
Badger mnyama mdogo aliye na rangi ya kijivu aishiye shimoni na anatoka usiku.
Swan aina fulani ya mabata maji.
A crab kaa.
Pony mnyama fulani jamii ya punda.
Gazelle mnyama jamii ya swala mwenye pembe ndefu zilizo jikunja.
A shark papa.
A cub mwana wa simba au chui au duma.
A calf mwana wa ng'ombe au tembo au nyati.
Tarpon Samaki mkubwa apatikanaye katika sehemu zenye joto zaidi katika bahari ya Atlantik.
Walrus aina fulani ya mnyama wa baharini.
A piglet mwana wa nguruwe.
Vixen Fox wa kike.
Tom tit aina ya ndege mdogo
Gull ndege fulani wa baharini.
Tern ndege wa baharini kama "gull" lakini kwa kawaida ni mdogo na mwepesi kupaa.
Teal aina ya mabata wadogo waishio mitoni na maziwani.
Viper aina ya nyoka mwenye sumu apatikanaye Afrika.
A gerenuk mwana wa twiga, swala kama twiga mtoto.
Cutler-fish samaki wa maji ya bahari ambaye anaposhambulia hutema maji maji meusi, ngisi
Wart-hog ngiri.
A hare sungura (mkubwa wa porini)
A mule nyumbu
A whale nyangumi.
A salmon namna ya samaki mkubwa mwenye nyama nyekundu.
Sardine samaki mdogo ambaye hupikwa na kutiwa ndani ya mafuta ya alizeti na kuuzwa
ndani ya makopo.
Porcupine nungu
Pelican ndege mwenye mdomo mkubwa sana, mwari.
An Owl bundi.
Python chatu.
wildebeest Kongoni, nyumbu.
Hunting dog mbwa mwitu.
Gecko aina fulani ya mjusi apatikanaye katika nchi za joto
An ibex mbuzi wa porini mwenye mapembe yaliyojizungusha.
Swallow mbayuwayu.
Terrapin kasa.
Oryx Choroa
Pangolin Kakakuona
Sable palahala
Sitatunga nzohe.
Bush baby komba
Topi nyamera
Ratel nyegere.
Spring hare kamengedere
Genet kanu
Enland pofu
Duiker kipoke, ndimba
Water buck kuro
Serval mondo
Penguin ndege fulani wanaopenda kukaa karibu na bahari walio na miguu mifupi na hawawezi
kuruka, wanasimama kama watu.
Bush buck mbawala au pongo.
Chimpanzee sokwe mtu.
Grant gazelle swala grant
Impala swala pala.
Vervet monkey tumbili
Pheasant ndege fulani mkubwa mwenye kishungi kwenye kichwa chake.
Anchovy samaki mdogo wa aina ya herrings atumikaye kwa kitoweo mwenye ladha mtamu sana
Coyote aina fulani ya mnyama kama mbweha aishiye Amerika.
Wolf mnyama jamii ya mbweha.
ukurasa mkuu wa masomo ukurasa mkuu wa majina (nouns)