Past progressive tense

Muhraja's après ski & nocturnal English language course

Tenses (nyakati)                               Home

  Tunapozungumzia tense hii, tunazungumzia kuhusu kitendo ambacho kilifanyika katika kipindi kilichopita lakini kilikuwa bado kinaendelea wakati mzungumzaji alipokuwa akishuhudia na kukiacha kikiendelea bila kujulisha kuwa kilikwisha, Hii ina maana kuwa, vilifanyika vitendo viwili, lakini kitendo kimoja kikaisha kabla wakati kingine kinaendelea, kwa mfano, Unakwenda shuleni, njiani ulipokuwa unapita uliona watu wakipigana, wewe kama mpita njia uliendelea na safari yako ya kwenda huko, utakapokuwa ukisimulia kuhusu tukio hilo utasema hivi

       "Nilipokuwa ninakwenda hospitalini, niliona watu wakipigana" Maandishi yaliyoandikwa katika rangi nyekundu yanaonyesha kuwa, kitendo kimoja kipo katika wakati uliopita uliokuwa ukiendelea (nilipokuwa nina.. ) na kitendo cha pili, (niliona..) huonyesha kuwa kitendo hicho cha kuona kilipita na kilikwisha kwa kuwa muonaji alipita na akawaacha hao wakipigana, kwa mfano huo hatujui kuwa walianza kupigana wakati gani kwa kuwa hapa mpita njia aliona watu hawa wakiendelea kupigana lakini hajui walianza wakati gani na walimaliza wakati gani, bali tunachojua ni kuwa, mpita njia aliwaona wakiwa wanaendelea na zoezi lao na akawaacha wakiwa bado wapo katika zoezi hilo.

  Kabla hatujatoa maelezo mengi zaidi katika kuelezea tense hii, inabidi tuone muundo wake kwa ufupi;

 Past progressive tense hutengenezwa au huundwa na past tense ya verb "tobe" + present participle.

Subject past tense of verb tobe

present participle

They  were walking
She  was driving.
We were cleaning...

Affirmative (maelezo)

 

 

She

was

typing.

Negative (ukanusho)    
We were mopping. 
Interrogative (Maulizo)    
Were they coming?
Interrogative negative (Maulizo makanusho)
Weren't you playing?

 I:.  Matumizi makuu ya tense hii;

      Kama tulivyokwisha ona hapo juu, past progressive hutumika sana kwa vitendo vilivyopita ambavyo viliendelea muda wakati fulani lakini ule wakati wa kwisha kwake haujulikani au sio muhimu kwetu kuujua. Inawezekana ikaelezewa kama kitendo ambacho hakijulikani wakati wake wa kuanza (yaani kilianza kufanyika wakati gani na kilikwisha wakati gani:

  II:   Tense hii hutumika bila kiambishi chochote cha wakati, yaweza ikaonyesha "gradual development", kwa mfano;

     "It was raining"                                "The car was running"

III: Hutumika kurejea wakati kabla wakati wa kudhihirika kitendo chenyewe, yaani inaelezea kitendo ambacho kilianza kabla ya wakati huo na kikawa kiliendelea baada ya wakati huo na hata wakati wa kukiongea inadhihirisha kuwa kilikuwa hakijaisha au hakijakamilika. Mfano

  "At 13:00 hrs they were having lunch"  (Saa saba mchana walikuwa wanakula chakula cha mchana)

      Hili humaanisha kuwa, saa saba mchana watu hao walikuwa bado wanaendelea kula na huenda wamefika katikati ya mlo wao. Na hii ina maana walianza kula kabla ya saa saba mchana na wakawa wanaendelea.

  Ikiwa tutarejea katika maelezo hapo juu, ambayo tulisema, vitendo viwili vikifanyika na kimoja kikaisha kabla ya kingine kama hivi hapa chini, tunaona kuwa kuna kiambishi cha wakati kinaingia, hebu tazama mfano huu;

   "When I was going to school I saw Hilal riding a bicycle."

        Tukiwa tunatunga au tunatumia sentensi za namna hii, tunafikisha wazo au dhana kuwa, kitendo katika wakati uliopita uliokuwa ukiendelea (past progressive tense) kilianza kabla ya kitendo cha wakati uliopita (Yaani kitendo chenye verb ya past tense na kuna uwezekano kiliendelea baada ya kitendo hicho. Hapo utaona kuwa, kitendo kilichokwisha ni "saw" (nilimuona)na kitendo kilichokuwa kikiendelea ni "riding" (kuendesha baiskeli)

  Twaweza kutumia past progressive katika maelezo. Kumbuka kuwa mkusanyiko wa maelezo katika (Past progressive) ukiwa na masimulizi (simple Past tense)

      "The sun was shining and the birds were singing as the elephant came out of the jungle. The other animals were relaxing in the shade of the trees, but the elephant moved very quickly. She was looking for her baby, and she didn't notice the hunter who was watching her through his binoculars. When the shot rang out, she was running towards the river..."

 

Past progressive ikiwa na neno "always" hutumika katika kuelezea vitendo vilivyokuwa vikijirudia rudia katika past progressive tense, vile vile hutumika kwa vitendo vinavyosemekana kuwa vilikuwa vinaendelea kipindi hicho.

  Tazama mifano hapo chini;

  The man was always stealing my properties.

  Hapo ni kwa vitendo vilivyokuwa vinajirudia rudia.

 He was always drinking.  (Vitendo vinayoonekana kuendelea kufanyika)

     Aina hii ya vitendo mara nyingi huwa ni vile ambavyo huwaudhi waongeaji, lakini sio kuwa lazima viwe tu ni vitendo vya kuwaudhi waongeaji, Mfano kama hapo juu

mtu akisema

 "She was always playing" humaanisha kuwa mtu huyo hutumia wakati wake mwingi sana katika kucheza. 

  Amma katika ile ya kujirudia rudia kama tulivyo kwisha itaja hapo juu huwa; kwa vitendo vilivyokuwa vinajirudia rudia na vyenye maudhi kwa muongeaji au kinaonekana kwa muongeaji huyo kuwa ni kitu cha kipuuzi kisicho na msingi wowote katika maoni ya muongeaji. 

    Juma was always spend pees at the ground.    (Juma alikuwa akikojoa kojoa  uwanjani {ovyo})

 Kwa kuendelea kusoma somo hili, Click hapa

                            Kabla hatujafunga somo letu hili  Zingatia Haya kwa ufupi

2. Past progressive na kazi zake.

         past continuous hueleza kitendo au tukio katika kipindi cha wakati kabla ya sasa, ambacho kilianza wakati uliopita na kilikuwa kinaendelea wakati wa kukiongelea, kwa maneno mengine, hueleza kitendo kilichokuwa hakijakamilika au kilichokuwa hakijaisha wakati uliopita.

Hutumika:

  •  Mara nyingi kueleza background ya kisa au masimulizi yaliyoandikwa katika past tense, mfano.

  • Kuelezea tukio au kitendo kisichokwisha ambacho kilikatishwa au kiliingiliwa na kitendo kingine au tukio lingine: "I was having a beautiful dream when the alarm clock rang."

  • Huelezea mabadiliko ya kimawazo: e.g. "I was going to spend the day at the beach but I've decided to go on an excursion instead."

  • Kwa neno 'wonder', hutumika ndani ya tense hii kufanya  very polite request: mfano: "I was wondering if you could baby-sit for me tonight."

Mifano zaidi:

a. They were waiting for the bus when the accident happened.
b. Caroline was skiing when she broke her leg.
c. When we arrived he was having a bath.
d. When the fire started I was watching television.

Zingatia: zikiwa na verbs sio kawaida kutumiwa katika muundo wa progressive  

 

  By Muhseen bin Rajab

Monday, August 26, 2002