Muhraja's après ski & nocturnal English language centre

future progressive tense.

                          Home             

        The future continuous tense (wakati ujao unaoendelea)

           Tense hii hutumika kuonyesha matendo mawili ambayo yatafanyika katika kipindi kijacho (mustaqbal)

ambapo panatokea kuwa kitendo cha kwanza hukatishwa na kitendo cha pili, nayo tense hii ina sehemu mbili,

sehemu ya awali, hii imebeba simple future tense ya verb to be.

I shall be

he will be

she will be

It will be

we shall be

They will

You will.

sehemu ya pili:  Hii ipo katika continous tenses zote, present participle ya verb husika yoyote hutumika katika sentensi.

mifano:

I shall be reading when he arrives.

  Hii hutueleza kwamba vitendo viwili vilivyofanyika katika kipindi kilichopita na kingine kitakuwa kimeanza kabla ya kingine. katika sentensi hiyo hapo juu basi, kitendo cha kwanza ni "shall be reading" kimeingiliwa na kukagonganishwa na kitendo kingine (cha pili) "arriving".

  Kitendo hicho cha pili au kitendo kingine kinachochukua nafasi kama hii ya pili huwa ni lazima kiwe katika simple past

   tazama mifano zaidi hapo chini;

I shall be waiting for the result at my home when I finish off my last examinations.

We shall be learning Mathematics when you reach there.

You will be cooking when your brother arrives.

When Hilal comes, they will be making all thing clear.

They will be going to the meeting before we reach there.

We shall be working for our last examinations when you come to visit us.

Abdul will be speaking to them next month at the time we usually at our work place.

They will be trying to solve the problem.

We shall be watching TV.

He will be listening to radio.

She will be reading.

Abdur Rauuf will be doing it.

I shall be talking to them.

  Kutokana na hayo yote hapo juu, na tuone mifano michache ya future continuous tense ya lugha ya Kiswahili kabla hatujaingia katika maelezo machache na kufunga somo letu hili.

Nitakuwa nikiendelea kula wakati huo atakapokuwa anafika nyumbani.

neno 'ta" katika Kiswahili lililopigiwa mstari, linaonyesha wakati ujao, neno "ki" kama lilivyopigiwa mstari litakuwa laonyesha wakati unaoendelea na neno "ana' linaonyesha wakati uliopo, lakini, hapa inaonyesha kuwa kitendo kilichoanza kabla ya kingine ni "kula" na kikaja kikagongana na kingine ambacho ni "kufika"

  Inaweza kuonekana sasa kuwa, kila tense ina kazi yake maalum ya aina yake inayoifanya, kwa ufupi ni kuwa, tense hii inaweza vile vile kutumika katika kueleza kuwa wakati fulani kitu fulani kitakuwa kikiendelea kufanyika, mfano

 Abdul Majid:   "Unafikiri ukifika Abdus Swamad atakuwa (akiendelea) kufanya nini?"

Abdul Maalik:   "Nafikiri atakuwa akiendelea kufua nguo zake"

  Kwa Kiingereza nikuwa maneno hayo au sentensi hizo katika mazungumzo kati ya Abdul majid na Abdul Maalik zinakuwa hivi.

Abdul Majid:   Do you think what Abdus Swamad will be doing?

Abdul Maalik: I think he will be making laundry (washing his clothes).

    Bila shaka sasa utaweza kutofautisha kati ya tenses uliyosoma na nyingine ambazo tayari au bado hujazisoma humu.

   Kumbuka-: Kannuni katika tense hii juu ya kutengeneza affirmative sentences ni kama ifuatavyo:

Subject + will/shall  + be + present participle

 Katika kutengeneza interrogative sentences, kanuni ni kama ifuatavyo:-

Will/ Shall + subject + be + present participle.

mfano:-

 Will the man be reading his mail.

Will you be trying to solve the problem?

     Nakutakia masomo mema na ninakuhimiza utuandikie kama hujaelewa au una maswali.