Do kama ordinary verb

  Do, kama ilivyo "have" Inaweza ikatumika kama ordinary verb (Verb ya kawaida). kisha huunda sentensi zake za negative na interrogative katika simple present na past kwa kutumia neno do/did: Mfano;

    I don't do (I do not do)        Do you?          Don't you do?

    He doesn't do.                    Did he do?      Doesn't he do?

  Yaweza ikatumiwa katika miundo ya kuendelea (Progressive forms) au hata katika simple forms.

  What are you doing now? ~ I am writing my homework.

   What are you doing tomorrow? (wakati ujao wa karibu)

   What does Nur do in the morning? (Tabia)

  How do you do? sehemu zote mbili zinazojitambulisha husema baada ya kwish jitambulisha (Kwa masomo zaidi juu ya hili angalia kwenye salaam) mfano;

    Hilal: Mr. Abdu, may I introduce my wife Nur? Wote Nur na Abdu watasema baada ya kutambulishwa

    "How do you do?" Chanzo cha neno hilo kilikuwa ni kumtakia mtu hali kuhusu afya yake. sasa ni salamu rasmi.

     Tazama matumizi mengine ya neno "do" kama yalivyo hapo chini,

   Would 100,000/= shillings do? (=Je, shilingi 100,000/= zingetosha), Mtu aliye ulizwa atatakiwa kujibu bila kutumia neno "do" na kusema kama haitoshi ~ No, It wouldn't. I need more 50,00/=

 Kwa maana hiyo basi, neno hilo katika sentensi hiyo lina maana ya "kutosha" na zipo sentensi ambazo neno hilo hutumika kama "a kufaa/inafaa" Mfano; I haven't a pen, Will a pencil do?" (=  Sina kalamu ya wino, je kalamu ya risasi inafaa?)

 Mengine ni kama "What do you do for living?" (Unafanya nini katika kuendeleza maisha yako/kazi) ~ 

 I am an electrician.

 How is the new born doing? (Anaendeleaje mtoto mchanga).

 Tunakutakia kila la kheri.

By Muhseen bin Rajab and Hilal Shukri. (canoksan and hilal)

Tuesday, September 03, 2002