|
|
PRESENT PERFECT NA SIMPLE PAST. kila wakati twatumia
present
perfect wakati wakati wa kitendo sio muhimu kwetu kuujua au haukutajwa.
Fananisha:
Kuna pia mielekeo tofauti ambayo mara nyingi huwa ni muhimu kuliko kidokezo cha wakati "What did you do at
school today?" ni swali linalohusu shughuli, na linaonyesha kuwa muda wa
shule umekwisha.hili lina maana kwa Kiswahili kuwa "Ulifanya nini shuleni leo".
(Wakati uliopita) PRESENT PERFECT ikiwa inafuatiwa na maneno kama 'ever, never, already, yet' Kabla hatujaendelea na mada yetu hii, yabidi kurejea katika maana halisi ya maneno haya kwa Kiswahili, ieleweke kwanza kuwa, maneno "Ever", "Never", "Already", na "Yet" ni vielezi Adverbs yaani vielezi ni maneno yanayo sifia verbs. Adverbs (vielezi) hivi vina kwa mada hii vina maana kama ifuatavyo kwa Kiswahili "Ever" =wahi, never= kamwe,(hata siku moja), abadan, Already = zamani,tayari, zama. Yet = bado. Adverbs ever na never huelezea wazo au kudokeza tukio la wakati usioeleweka (Usioelezeka) kabla ya sasa. Mfano; "Have you ever been to Zanzibar? "Have you ever eaten ugali?" (Je, umeshawahi kula ugali?) "Have you ever visited Dar es Salaam? 'Ever' hutumika
'Never'
Humaanisha "hapakuwa na wakati kabla ya sasa kufanya kitu fulani" na iko sawa na
kusema kwa kutumia kifungu cha maneno "not ......ever; mfano; I have never visited Nairobi.
Already na yet: Already
hurejea kitendo ambacho kimefanyika katika wakati
kabla ya sasa ambao haukutajwa. hudokeza kuwa, haihitajiki kurudiwa rudiwa.
Mfano. Hutumika pia katika
maswali:mfano; yet
hutumika katika maelezo ya makanusho na maswali
kumaanisha (bado) ndani ya kipindi cha wakati kabla ya sasa na sasa. bado hadi
sasa, mfano.
PRESENT PERFECT + for, since Kutumia present perfect, twaweza tukaelezea kipindi cha wakati kabla ya sasa kwa kuzingatia wakati wa kudumu kufanyika kile kitendo (Mfano, saa moja, masaa matatu, mwezi n.k) ikiwa imefuatiwa na neno "for" + kipindi cha wakati huo au kwa kuzingatia wakati wa kitendo hicho0 kuanza ikiwa imefuatiwa na neno since + tendo katika muda wake. For + kipindi cha wakati wa kufanyika kwa tendo :
Since + tendo katika muda wake tangu kuanza: Since he left school, he has drunk liquor. Since we launched the attack here, many people have fled.
Mifano zaidi: present perfect ikiwa na neno "for":
present perfect na neno "since":
Kumbuka! kAMA ULIVYOONA KATIKA BAADHI YA SENTENSI NI KUWA; Present perfect huweza kutumika kwa vitendo vitokeavyo katika kipindi kisichoisha. Sio hivyo tu, bali kipindi hicho kisichokwisha chaweza kuonyeshwa kwa "Today" (leo), this morning, this afternoon n.k Kumbuka kuwa present perfect yaweza kutumika na "This morning" hadi saa moja kamili hivi, kwa sababu baada ya "This morning"huwa ni kipindi kamili na kitendo kitakachotokea nje ya hapo yabidi kiwe katika simple past Ikiwa kuna kijana aitwaye Tom na tunamuelezea kufanya kitendo alichofanya kabla ya saa tano na sisi tunaongea wakati huo saa tano itakuwa hivi; Mfano, (Saa tano kamili asubuhi) utasema " Tom has rung up three times this morning." (Saa nane mchana) "Tom rang up three times this morning" Tazama sentensi ya kwanza na ya pili, ya kwanza ni kwa kuwa kitendo tangu kifanyike haijapita muda wa saa moja tangu kiishe, tumekiongelea, na ya pili ni kwamba umepita muda mrefu kidogo zaidi ya saa moja tangu kifanyike' Hadi kufikia hapa ninakutakia kila la kheri na uendelee kututembelea tena katika mtandao
Imeandaliwa na Muhseen na Hilal tarehe 27 June 2002 |