Make your own free website on Tripod.com

verb "to be"

Muhraja's après ski & nocturnal English language program

Katika somo letu leo tutazungumzia "Verbs" zijulikanazo kama "Auxiliary verbs" (yaani vitenzi visaidizi)

  Katika Lugha ya Kiingereza, tuna vitenzi visaidizi ambavyo vinafanya kazi kama vile tulivyo navyo katika Kiswahili, ingawa wakati mwingine twaweza kuona tofauti kidogo sana katika matumizi, lakini sio ya kutufanya tushindwe kuilinganisha na ya Kiswahili.

verbs  hizo ni kama

 to be, shallwill, can, may, have,

  Tutaanza moja kwa moja na "Verb "to be" yaani "kitendo "kuwa".Kwa Kiswahili, verb hii huitwa tendo kuwa'

"Verb to be" hubadilika kutokamna na personal pronoun unayoitumia, mathalan

I am a boy                                  mimi ni mvulana

You are a girl                             wewe ni msichana

He is a bad boy.                         yeye ni mvulana mbaya.

She is Mariam                           yeye ni Mariam.

It is twelve O'clock                    Ni saa sita kamili.

They are thieves.                       (wao) ni wezi.

We are teachers.                       Sisi ni walimu

maneno yaliyoandikwa kwa italic ni maneno yanayoonyesha verb 'to be". (tendo kuwa), kwa nini imeitwa verb "to be". hii bila shaka ni kwa sababu inaonyesha hali ya kuwa, mfano "fulani ni mwalimu'  (kawa mwalimu)

Mifano mingine ni kama;

Somebody is sick                            Fulani ni mgonjwa

Hilal is a student                              Hilala ni mwanafunzi              (Hali ya kuonyesha kuwa ni "is" = ni.

  Tukiwa tunataja watu wawili, (yaani They) verb "to be" ambayo ilikuwa kwa mtu mmoja ni "is" hugeuka na kuwa "are" ila ukumbuke kuwa personal pronoun "you" ndiyo pekee ikiwa kwenye umoja au wingi haibadiliki "verb to be" yake, yaani, muda wote itakuwa "you are" Hizo pronouns zingine zitabadilika badala ya "is" na kuwa "are" zikiwakilisha wingi. Mifano:

Hilal and Canoksan are cronies.                 Hilal na Canoksan ni marafiki wa karibu.

             John and Ramson is a students,         haya ni makosa, bali utasema

             John and Ramson are students.

            Negative sentences. (=Sentensi za kukanusha)

   Hizi ni sentensi za kukanusha juu ya jambo kwa kutumia neno "Sio" ambalo kwa Kiingereza ni "Is" kwa mtu mmoja na "are" kwa wengi, sheria ni kama hiyo hiyo iliyotajwa, ispokuwa unaongezea neno mbele ya verb "to be" neno  "not"

Mathalan;

I am not a boy                                               Mimi sio mvulana.

You are not a girl.

John and Ramson are not students.

Amma sentensi ambayo hayana kukanushwa kwa kuwekewa "not" au "no" hujulikama kama "Affirmative sentences". Mifano mingi nimetoa hapo juu. Na kinyume cha "affirmative" ni "negative"

  Pia tunaweza kufupisha badala ya kutamka kama ilivyo verb hii tunatamka kwa kuifupisha, na yenyewe ni kama hivi

I am                 (I'm)

You are            (you're)

He is                 (he's)

She is               (she's)

It is                  (it's)

We are           (we're)

They are         (they're)

    Interrogative mood  (Maulizo)

Ikiwa katika hali ya kuuliza swali, verb "to be" hubadilika na kukaa mwanzo kabisa wa sentensi, kama ifuatavyo

  Are they students?                                      je wao ni wanafunzi?

 Are you Husayn?

 Am I your schoolmate?

  Licha ya hivyo, tunatumia sana maswali kama haya lakini kwa ufupisho katika karibu kila lugha, katika Kiswahili mfano.

Mimi ni baba yako, au siyo? Basi katika Kiingereza ni vivyo hivyo, tunaita mada hii "Tags questions" ambazo tunatumia vifupisho vya verbs "to be" kama tulivyoonyesha hapo juu ikiwa tunakanusha kwa kusema "not"

nazo ni kama ifuatavo;

I am not your father, am I?

You are John, aren't you?

He is a policeman   isn't is"

She isn't a driver, is she?

They are our brothers, aren't they?

We are Muslims, aren't we?

Kumbuka kuwa, kama katika sentensi upande wa kushoto ni kukubali, basi question tag yake huwa kni kukanusha, na kama ni kukanusha basi huwa ni kinyume chake, angalia hapo kwenye sentensi ili ujue zaidi.

mazoezi;

badilisha kwa Kiingereza sentensi zifuatazo;

Mimi ni karani.

Mimi na wewe ni wanafunzi.

Hassan na Husayn marafiki.

Yusuf na Ahmad ni watundu.

mtoto huyu ni mwenye kiburi.

 

Tumia maneno yafuatayo katika kutunga sentensi zako.

Clerk           karani

Student       mwanafunzi.

friends       marafiki.

Arrogant   mwenye kiburi.

 Kurudi katika ukurasa wa mkuu click hapa