Make your own free website on Tripod.com

English main page, Jisomee Quraan, Sikiliza Qur-aan, Jifunze computer; Kuhusu mimi

Matumizi ya neno "have" (sehemu ya pili)

 kama tulivyoona mwanzo kuhusu matumizi na maneno have na get na kuyachambua kidogo kwa undani, leo tutaona kwa juu juu kuhusu maneno have na get zikiwa katika kufanya kazi pamoja katika sentensi moja, hata hivyo sehemu hii nitaongelea kidogo "have" kama kitenzi cha kawaida. Have kama kitenzi cha kawaida kama tulivyoona mwanzoni (Katika sehemu ya kwanza) tulitaja maana kadhaa, ikiwa ni pamoja na kumiliki na pia kuteseka au kutaabika (kwa ugonjwa, udhaifu, maumivu, ulemavu n.k). Tazama mfano hapa chini. Have you got flu? ~Yes. I have

 Kumbuka kuwa tulizungumzia kuhusu maneno mawili ambayo ni "have" na "get" na tukayachambua hadi tukaona kuwa kwa katika mahali pengine hufanana katika matumizi. Usiogope baada ya kuona tumetumia "have got" pamoja, ambayo pia unaweza kusema "have" badala ya kuongeza "got".  Kabla sijatoa mifano yoyote, inawezekana wewe msomaji ni mwanafunzi ambaye ni (beginner) ambaye ndiye unaanza kusoma lugha ya Kiingereza. Sasa nikutoe kidogo ugumu kwa kukueleza tofauti kati ya "have" na have got" ambayo ipo katika mfululizo wa masomo yetu ya neno "have" na ninaamini kuwa maneno haya yaweza kukuchanganya mwanzaji wa kujifunza lugha hii. Kitu cha kwanza ambacho ningependa kukufahamisha cha muhimu ndugu muanzaji ni kuwa, uelewe kuwa maneno "have" na "have got" hutumika katika umilikishaji. Mfano:-

 Badru has got a beautiful bag au Badru has a beautiful bag. (Yaani Badru analo begi zuri)

 Mifano hapo juu tumeona kuwa yote inaeleza kumiliki. Kumbuka kuwa have peke yake (Bila neno "got") inatumika tu pale tunapoongelea (tunapozungumzia) kuhusu vitendo. Tuone mfano;- I usually have breakfast at 7 o'clockSIO I usually have got breakfast at 8 o'clock. (Kila wakati nakula istiftahi/kifungua kinywa saa 1 (moja) kamili asubuhi. Hapa tunaongelea "have" katika vitendo (Kutenda). Na sio kumiliki kama tulivyokuwa tukitoa mifano hapo juu.

 Kumbuka kuwa, katika eneo hili mfumo wa maswali ya wakati uliopo (Simple present) maswali huundwa kutokana na neno (Auxiliary) "Do" kama inavyoonyesha hapa:- Do you have a fast internet connectivity? SIO Have you a fast internet connectivity? Kumbuka kuwa tunapoongelea simple present (wakati uliopo) tunaongelea vitendo vinavyojirudia rudia (au vya kawaida) ambavyo huwa ni kama tabia. (Do you often have headache? (Je, wewe mara kwa mara wajisikia maumivu ya kichwa?)~ No. I don't have

*Kitu cha kuzingatia: Ikiwa katika sentensi hakuna kidokezo cha vitendo vya kujirudia kama kitabia (habit). Miundo ya maneno "have not (got) na have you (got) ni ya kawaida sana kutumika Uingreza (British English), ambapo katika nchi nyingine zinazoongea Kiingereza (Hususan America) hutumia muundo wa neno "do". Muamerica anaweza kusema akitaka kukuomba msaada. Can you help me now? Do you have time? na katika eneo hili Mwingerza atasema. "Can you help me? Have you got time?" Kumbuka sana kuwa tunaongelea haya hapa mahali ambapo hakuna hata kidokezo cha vitendo vya wakati uliopo/Vya tabia. 

 * Tena maneno haya "have" na "Have not" hutumika tu katika present tense (wakati uliopo). Tumia neno "have" (tu bila got) kwenye wakati uliopita past simple na future (wakati ujao). Mfano:- He had a big and beautiful house. na SIO He had got ....

* Tumekuwa wengi wetu tukitumia vifupisho vya neno "have" katika sentensi za maelezo (katika sentensi za kukubali, yaani affirmative.) badala ya kuzitumia tu katika sentensi za kukanusha kama inavyokubalika au kuzitumia katika "have got". Mfano:- I have very fast computer. SIO I've very fast computer.  

  Natuangalie kiufupi tu katika grammar (Namna ya kuunda sentensi hizi) kama ilivyo hapa chini:- 

Katika Positive sentensi (Sentensi za kukubali) tukitumia kama subject (I, you, we, they have got). Nikisema sentensi za kukubali nina maana kuwa ni sentensi kama hivi:- Sharif has got a new car (Sharif kapata gari jipya~ Sentensi hii hukubali) lakini sio sentensi za kukataa ambayo mfano wake ni Sharif hasn't got a new car (Sharif hajapata gari jipya ~ Sentensi hii hukataa, yaani hukanusha). Na sasa tuangalie sentensi za kukubali zinavyofanya kazi na neno "have" na 

Mfumo ni     Subject + have + got + objects

                     They  have got a new computer (Hufupishwa) "They've got a new computer". Sasa na tutizame katika nafsi ya tatu umoja ambapo ni maneno kama He, she, it has got

 Mfumo:- Subject + has + objects (Zikiwa katika positive/ sentensi za kukubali)

                He   has got a new computer. (hufupishwa kwa) "He's got a new computer.

 Hapo juu tumeona mfano wa neno "have got" katika mfumo wa kuliandika kwa kufupisha, sasa tuone kidogo tofauti kati ya "have got" na "have" peke yake. Tunaingia katika kuzungumzia "have" katika positive (Affirmative)

  I, we, you, they have

Mfumo:- Subject + have + object

              They have a new computer. (Kufupishwa hapa kwa have hakuna). na ukisema They've a new computer hapa ni makosa, sio katika grammar ya Kiingereza. Hivyo pia ndivyo ilivyo katika nafsi ya tatu umoja. Nayo pia nainukuu muundo wake na kisha kuieleza.

       He, she, it +  has + object

      She has a new computer. (Hapa hakuna kifupisho kinachokubalika kama mbavyo pia tuliona hapo juu). Hutaweza kusema "She's a new computer" Kumbuka ukisema hivyo unamaanisha kitu kingine kabisa na kama huna maana hiyo basi ujue sio sahihi kufupisha kwako.

  Kabla hatujazama kidogo katika somo letu hili la "have" sehemu ya pili, inatubidi kuendelea kutofautisha kwanza maneno "have" na "have got" katika mfumo wa sentensi za maswali sasa. Tuanze na "have got"

Maswali.

Muundo wake ni (?) + have + subject + got?. kwa mfano.

 Maswali (Interrogative) I,we,they,you have got

     Mfano:- How many computers have they got? (Hapa hakuna kifupisho). Na sasa tuangalie upande wa Pronouns (Viwakilishi vya nafsi) ya tatu na namna vinavyofanya kazi katika eneo hili.

Maswali: She, he, it has got. (Mfumo wake ni (?) + subject + got.)

  Mfano:- How many computers has he got? Bila shaka hadi hapa tutakuwa tumepata kidogo picha halisi ya haya maneno mawili ambayo yamekuwa katika mfululizo wa somo letu hili kama maneno yanayoingiliana katika baadhi ya maeneo tuliyoyapitia hususan katika toleo la mwanzo. Na sasa tuitizame kidogo mada yetu hii tukiwa tunaiona "have" na "have got" katika mfumo wa sentensi za ukanushaji (Negative form) 

Kukanusha: (Negative) I, You, We, They HAVE GOT
Subject + have + not + got + objects
We have not got a computer (Hapa tunaweza kufanya vifupisho (Contraction): na tukaandika We haven't got a computer. Tukiendelea na mada yetu hii, katika kuweka nafsi ya tatu umoja katika kueleweka juu ya eneo hili. Tazama mifano hapa chini. 

Kukanusha (Negative) He, She, It HAVE GOT
Subject + has + not + got + objects
She has not got a computer. (ufupisho) Contraction: She hasn't got a computer.

(Kukanusha) Negative I, You, We, They HAVE
Subject + do + not + have + objects
They do not have a computer. (Ufupisho) Contraction: They don't have a computer.

 (Kukanusha) Negative He, She, It HAVE GOT
Subject + does + not + have + objects
She does not have a computer. (Ufupisho) Contraction: She doesn't have a computer. 

  *Vidokezo:

Katika Question tags. Neno get haliwezi kamwe kuonekana katika majibu mafupi ya maswali katika Question tags. Tazama mfano: Have you got a computer? ~ Yes. I have.

He's got the most reliable computer, hasn't he? Kitu kingine kutoka katika sehemu ya kwanza tulivyosoma, ni katika matumizi ya neno "have". Tuangalie kidogo katika kufanya marudio na kuweka wazi kidogo sehemu ambayo ilikuwa haikueleweka vizuri. 

 Tulisema "have" humaanisha kula na tulitoa mifano,pia ningependa kuongezea kuwa neno hilo lina maana pia kutoa, kuwa katika hali ya matatizo, pia furaha. Mfano: "They are having a party tomorrow" (Kwa kuonyesha entertainment) 

 Twaweza kutizama kwa haraka haraka

Have na got huwa kama verbs (vitenzi vingine katika kutengeneza sentensi zake za maswali na kukanusha hutengenezwa kutokana na neno "Do" au "did" na vile vile huweza kutumika katika continous tense (Wakati wa hali ya kuendelea). Tazama mifano

We are having a meeting early tomorrow. (Tunafanya mkutano kesho mapema) (wakati ujao wa karibu)

She is having twenty students to join his class next month. (wakati ujao wa karibu)

I can receipt my guest. I am having a bath. (wakati uliopo) Present.

You have mathematics period at 10:00. Don't you? (tabia au ratiba).