Muhraja's après ski & Nocturnal Swahili English program -C

Muhraja's après ski & Nocturnal Swahili English program -Can. 

  katika mada yetu sasa ni kuhusu neno Can

Can ni auxiliary verb, amayo hujulikana kama 'Modal auxiliary verb'. Tunaitumia  "can" ku:

Can hutumika katika kuomba ruhusa kama tulivyoona katika neno may. Tunatumia can kuongelea kuhusu vitu ambavyo vinawezekana kama ambavyo unaona kwenye jedwali hapo chini, mfano

She can drive a car (Yeye anaweza kuendesha gari).

I can speak Somali (Naweza kuongea Kisomali)

I can't find my pen

      Muundo wake

Can hutumika kwa nafsi zote katika present na future.

Could hutumika tunapoongelea past (Wakati uliopita) na conditional 

 Katika jedwali hapo chini linaonyesha kwa ufupi namna ambavyo can itatumika katika hali zilizo tajwa kwenye jedwali hilo.

Subject Neno "Can" (Bare Infinitive) main verb
You can  tell
She
Hilal
can
can
cook
drive

Affirmative (Maelezo)

We  can play
I can ski

They

can

study

Negative (Ukanusho)

He  can not (Can't)  dance
We can't sleep

You

can't

work

Interrogative (Maulizo)

Can she assist? 
Can they phone? 

Can

you 

share?

Interrogative negative (Maulizo makanusho)

Can't we bank?
Can't he type?

Can't

they 

play?

  

     Katika muundo mwingine, neno allow laweza kutumika,au be allowed. Neno can kila wakati hufuatiwa na bare infinitive (Infinitive bila neno "to") kama unavyoona hapo juu kwenye jedwali.

Can yaweza kutumika katika kuomba ruhsa wakati ujao au hata wakati uliopo:

A:  Nafsi ya kwanza:

     I/we can ni muundo wa kawaida sana kuonekana.

    I can spend money however I like. (Naweza/nina ruhsa ya kutumia fedha yangu nitakavyo). Kwa lugha nyingine ni kuwa, tunajua kwa Kiingereza kuwa neno ruhusa linaitwa "permission" hivyo tunaweza tukaifanya sentensi yetu iwe hivi; I/we have permission to spend money 

 I can leave the class room as soon as I finish my class works inaweza kuchukuliwa nafasi yake na neno "be allowed/allowed" kama tulivyokwisha taja hapo juu na hivyo ikawa ni "I am allowed to leave the class as soon as I finish my class work"

  Tunapozungumzia nafsi ya pili na nyinginezo, kama ambavyo tunaona hapo chini, yabidi kuzingatia sana maelezo yanayotolewa humo ili usijichanganye mwenyewe.

You can take my book   = Nakuruhusu uchukue kitabu changu (=I allow you to take my book)

She can call me anytime = Namruhusu aniite wakati wowote. (=I allow her to call me anytime)

They can park here = nawaruhusu waegeshe hapa (=I allow them to park here)

They can't go home now =Siwaruhusu waende nyumbani sasa hivi (=I don't allow them to go home now)

You can't throw rubbish here =sikuruhusu kutupa takataka hapa (=I don't allow you to throw...) Sio kitu cha busara kutupa takataka hapa.

  Kumbuka kuwa, katika kuomba ruhusa, kama mzungumzaji anatumia negative interrogative ni kuwa anatumaini kupokea majibu kutoka kwa muombwaji ambayo yapo katika affirmative. Mfano;

Can't I stay here for all the time? (Siwezi kukaa hapa kwa muda huo wote?)

  Sio dhumuni langu kuongelea kila kitu hapa kwa wakati mmoja, ila dhumuni langu ni kukuwezesha kujua kuwa unapoongelea nafsi katika kutumia neno can, inabidi uelewe matumizi katika kila nafsi huathiri au hubadili vipi kitendo. Itazingatiwa katika mada yetu ambayo tulisoma juu ya neno may

Utaona kuwa neno may wakati mwingine humaanisha kuwa na (=haki ) kulalamika.Vile vile neno can huweza kutumika hapa: Mfano;

A boy can tell his parent about the cruel teacher. (Mvulana anayo haki ya kumweleza mzazi wake kuhusu mwalimu huyo mkatili). Mifano mingi tu inaweza ikapatikana pale ambapo tutataka kuitumia can kwa maana ya "kuwa na haki"

   Amma tukiingia katika past tense. kama tulivyotangulia kusema kuwa neno hili huwa ni "could". Tutakumbuka kuwa, tumeonyesha hapo mwanzoni kuwa, neno "can" hutumika katika kuomba ruhsa, Vile vile tujue kuwa, hata katika wakati ujao, neno hilo laweza kutumika katika kuomba ruhsa likiwa katika hali ya wakati ujao (Could). Mfano

 I couldn't join the school because I ........ (sikuruhusiwa kujiunga na shule hiyo kwa sababu .....)

  Na hii huweza kusemwa kama {"I was not allowed to join the school because I ...)

Neno could huweza kuelezea ruhusa ya kwa ujumla katika wakati uliopita,  wakati kitendo fulani kiliruhusiwa kufanyika na kufanyika twatumia maneno Was/were allowed badala ya Could: Kwa maelezo zaidi kuhusu could Click hapa

can: Kuomba na amri

  Mara nyingi twatumia can katika maswali kumuomba mtu fulani atufanyie kitu fulani. Hii sio swali haswa - hatuhitaji haswaa kujua kama mtu tunayemuomba anaweza kutufanyia kitu fulani, Tunamhitaji atufanyie kitu hicho! Matumizi ya can katika njia hii sio rasmi (hutumika sana baina ya rafiki na familia):

Mfano:

  Can: katika uwezekano

  Kwa ujumla, Can inaweza kumaanisha, "Inawezekana". mfano katika masuala ya ruhusa, (hii ni tofauti na aina nyingine za uwezekano ukilinganisha na vile ambavyo inaelezwa na may ):

 You can sit here (ina maana panafaa kukaa)

We can't pass by there on foot on account of robbers = Hatuwezi kupitia pale kwa miguu kwa ajili ya majambazi (Hapana usalama)