canoksanhilal home

Tenses (nyakati)

     Tenses ni maneno yanayoonyesha hali ya kitendo ya wakati wake uliofanyika, mathalan, katika Kiswahili, mtu akisema, alikwenda, anakwenda, atakwenda. Hayo yote ni maneno yenye maana moja. Lakini tofauti yake ni hali ya wakati wa kufanyika kwa tendo hilo.

  Katika lugha ya Kiswahili, inasemekana kuwa kuna tenses (nyakati) tatu, nazo ni

Wakati uliopo  (simple present tense)

Wakati uliopita (simple past) na

Wakati ujao  (simple future)

 

Vivyo hivyo ndivyo Kiingreza kilivyo, nacho kina tense za namna hiyo hiyo, tunajua kuwa kuna hali za tenses hizi, mfano,

ü      Hali ya kukamilika  (perfect tense), mfano: nimekula, kitendo cha kula kinaonyesha ukamilifu wake, yaani kimetimia au kimeacha athari hadi sasa hivi. (yaani kwa ujumla kitendo hicho kina uhusiano mkubwa na wakati uliopo ingawa kimepita

ü      Hali ya kuendelea  (progressive tense), mfano:ninakula, kitendo cha kula kinaonyesha kuwa bado kinaendelea wakati huu huu tunaozungumzia na bado hakijamalizika.

    Kumbuka kuwa, katika Lugha ya Kiingereza, mambo hayo yote yapo; kama unahitaji kujua somo miongoni mwa hayo, click katika mada inayohusika hapo chini;

 

 Katika mpangilio mzuri wa maelezo ya tenses hizi ni kama ilivyoonyeshwa hapo chini

Present

 

Simple present tense

Present perfect tense

Present progressive tense

 

Past

 

Simple past tense

Past perfect tense

Past progressive tense.

 

Future

Simple future tense

Future perfect tense

Future progressive tense.

 

 Kwa masomo mengine rudi katika ukurasa mkuu kwa kuClick hapa