Muhraja’s après ski & nocturnal English Program centre

Tenses                     Home

Simple future tense (wakati uliopita)

   Katika Kiswahili, itakumbukwa kuwa, tunapoongelea masuala ya mustaqbal (yaani ya wakati ujao) yabidi tunatumia  maneno kama vile "_ta_" kuonyesha hali ya wakati unaokuja. mfano tuchukue maneno kama kulia, kuandika, kusema n.k yatakuwa kama hivi:-

Atalia, ataandika, atasema na kadhaalika. hata kama utatumia nafsi ya aina yoyote, neno 'ta' ambalo kwa Kiswahili huchukua nafasi ya kuonyesha kitendo kijacho,  linachukua nafasi ya auxiliary verbs (vitenzi visaidizi) mbili ambazo ni "Will na Shall, Lakini kumbuka katika Lugha ya Kiingereza, maneno haya hutumika kutegemeana na nafsi uliyoitumia kama subject ya sentensi yako hiyo.

      Katika Lugha ya Kiingereza,  tuna maneno yanayofanya kazi inayofanywa na neno "ta" katika Kiswahili, Kwa Kiingereza yapo maneno kama hayo ambayo ni "shall' na "will". Maneno yote hayo yanaweza kutumika katika kueleza kufanyika  kwa Kitendo katika wakati ujao, nayo hayo maneno mawili yanategemeana na nafsi unayoiongelea kama subject ndani ya sentensi yako.

   "Shall" hutumika pale mtu anapotaja nafsi ya kwanza ("I" na "we") tazama mifano hapo chini

I shall try to check it soon.              ( Mimi nitalisimamisha mara moja)

We shall eat Pilau.                         (Sisi tutakula Pilau).

I shall do it by tomorrow.               (Mimi nitalifanya hilo kesho)

  "Will" hutumika kwa personal pronouns zote zilizobaki (yaani zote ispokuwa "I" na "we") lakini hata hivyo, kwa upande wa watumiaji wa American English wanatumia "shall" katika personal pronouns nyingine mfano wanasema

 He shall ......

  Ila napenda kuwashauri sana wasomaji waliopo Africa mashariki hususan Tanzania kuwe, kutokana na Kiingereza ambacho hata mitihani ya masomo inatolewa hasa kwa Kiingereza cha Uingereza (British English) ambayo yenyewe ndio inafuata mfumo wa kuzitumia kama huu ulioelezwa humu.

  Will

  Kama tulivyotangulia kusema hapo mwanzo kuwa personal pronouns zilizobakia zitatumia "will" katika kueleza kipande chake cha wakati ujao, mfano

He will go to Mozambique next week.              (atakwenda Msumbiji)

She will read her mails.                                    (Atasoma barua zake).

They will swim.                                               (wataogelea)

It will take too long to finish off the work.        (itachukua muda mrefu kumaliza kazi hiyo).

  Matumizi ya auxiliary verbs hizo katika hali ya kutunga sentensi katika hali ya maswali (interrogative form)

    Kama nilivyokwisha eleza katika baadhi ya tense kuwa, auxiliary verbs zinazosaidia kutengeneza sentensi ya tense fulani, ndio huwa neno la kwanza kuanza wakati ukitunga sentensi zinazokuwa katika hali ya maswali.

   Katika tense hii, mambo sio tofauti na yalivyo katika tense nyingine, ni mfumo uleule utakaotumika kutengenezea sentensi za namna hii. tazama mifano hapo chini;

Will Abdul go to Somalia tomorrow?

Will they come back soon?

Shall I do it?

Will he tell you about the thief?

Will it survive?

Will they play football?

   Itakumbukwa kuwa, katika kila lugha kuna question tags, na hizi katika lugha ya Kiingereza tumeziona namna zinavyofanya kazi kutegemeana na tense tunazozitumia, Amma katika tense hii, ni vyema tujue kuwa iko kama zilivyo tense nyingine, hii ni kwa sababu, auxiliary verb inayosaidia tense ya namna hii ndio huwekwa mwanzoni kabisa katika kutengeneza Question tag hii. Angalia mifano hapo chini;

  Kabla ya kuendelea na mada inabidi kuzidurusu baadhi ya hali ya hizo auxiliary verbs mbili

Shall not = shan't.

Will not = won't.

Sentense (startment)                                                     maana.

Affirmative form

 I shall claim him $2,500. Shan't I?                                        Nitamdai dola za Kimarekani 2,500 au sio?

We shall lose our purses. Shall we?                                       Tutapoteza pochi zetu, au sio?

He will put off this event, won't he?                                       Ataliahirisha jambo hili, au sio?

I shall pick out all English book from his table.                       Nitavichambua (kwa kuvitenga) vitabu vyote vya

                     Shall I?                                                            Kiingereza kutoka katika meza yake, au sio?

My son will give it to you, won't he?                                     Mtoto wangu atakupa, au sio?

Tuziangalie zikiwa katika Negative form., zinakuwa kama ifuatavyo;

Sentensi                                                                        Maana

I shan't forget what you told me, shall I?               Sitasahau uliyoniambia, au sio?

They won't take anything to us, will they?             Hawatatuletea chochote, au sio?

He won't tell you what I told him, will he?            Yeye hatakuambia niliyomueza, au sio?

    Tofauti ambayo yaweza kuonekana hapo juu, katika negative na affirmative ni kuwa, katika negative, huwa ille "not" iliyo katika sentensi haiwezi tena kuwekwa katika auxiliary verb husika, na ikiwa ni affirmative, kwa sentensi yake haina neno "not" basi itawekwa neno hilo katika auxiliary verb yake, yaani kwa ufupi ni kusema, sentensi ikiwa "She will not ( She won't)" basi kuulizwa kwake kutakuwa "Will she?"

  Na ikiwa sentensi ni kama "They will need to do so" itakuwa "Won't they?"

  Kwa kifupi tu ni kuwa, kila mada unayoisoma ni vyema ujitahidi kutunga sentensi katika kuweza kuihifadhi kichwani na vile vile yabidi uitumie katika mazungumzo yako. kabla sijamaliza mada hii, ningependa nikufahamishe baadhi ya maneno ambayo nimetumia humu.

 Shall =             ni neno linalotumika katika nafsi ya kwanza (I and we) wakiwa kama watendaji wanaotarajiwa 

                        kufanya kitu au jambo fulani katika kipindi kijacho.

Will =               ni neno linalotumika katika nafsi zilizobakia zikiwa kama watendaji wanaotarajiwa 

                        kufanya kitu au jambo fulani katika kipindi kijacho. (nafsi hizi ni zote isipo kuwa I na We)

Next week =   wiki ijayo, juma lijalo.

Read = soma,  mfano "read mails" = soma barua. finish = maliza/ malizia. finish off = malizia kabisa.

Go = nenda,  forget = sahau.  tell = ambia. lose = poteza. swim = ogelea.    told =  (..liambia)

Come back = rudi. come back soon = rudi mara moja,  forget = sahau. anything = chochote.

Do = fanya. survive = kuishi. about = kuhusu. claim = kudai.

   Hadi hapo, kama kuna maneno zaidi jaribu kutumia kamusi kwa Kucklick hapa

Ikiwa kuna maswali au kama hujaelewa baadhi ya vitu, jaribi kuwasiliana na mimi kwa anuani hii

 canoksan@yahoo.com au hilalshukri@yahoo.com