Dictionary  home Qur'aan Islamic studies  home English main page sentences pattern 

Muhraja's après ski and nocturnal English program center -  Sentence patterns

  Sentences pattern two

       Labda ingekuwa ni wakati muafaka sasa kuweka wazi kuwa, hizi sentensi patterns kuwa makundi haya kama tulivyo ya gawa na kuyaita pattern One, two na kuendelea ni katika kurahisisha somo letu tu ndio maana tunayataja kwa kuyaita majina moja moja ili iwe nafuu kwa mwanafunzi wetu na hatimaye ayajue kirahisi na kwa usahihi ili azungumze na kuandika lugha sahihi, Tukiendelea na somo letu hili, hebu tuione mifano michache na ni vizuri kila mara tunaposoma pattern moja hadi nyingine tujaribu kuangalia tofauti ya pattern iliyopita na iliyopo; Tuone mifano hii;

  The boy in the blue hat is outside.

  The book that you said you'd lost is on the table.

    Tukirejea katika maneno ya msingi yaliyojenga sentensi hizi ni yale yaliyoandikwa kwa italic, nayo ni haya

"Boy is outside."

   Ni wazi kuiwa tunapoiangalia sentensi pattern hii kwa karibu zaidi tutaona kuwa ina tofauti za sentence pattern one katika njia mbili, Namna ya kwanza ni kuwa, ina adverb (kivumishi) kama sehemu ya sentence pattern. Hata hivyo adverbs (Vivumishi)  pekee uwezavyo kuvitumia ni kama vile outside, up, there, underneath, n.k

  Pia unaweza kutumia tu verb "to be" katika miundo yake kutegemeana na pronoun au noun unayoitumia katika sentence pattern One waweza ukatumia mamia ya (vitenzi) verbs. Sasa hapa ni mifano zaidi ya sentence pattern two (Mada tunayoendelea kuisoma sasa hivi).

  (Your) book is underneath.

  (The) girl was downstairs.

   Maneno kwenye brackets katika sentensi hizo haya tengenezi sehemu yoyote ya msingi ya sentence pattern, kazi za maneno hayo ni kuieleza tu sentensi.

   Vifungu maneno katika sentence pattern two.

    Hapa tuone mifano michache ya vifungu neno katika pattern hii,

   (The) thief was near the shop.

   (The) shopkeeper was in the shop.

   Hapa vifungu neno vimekaimiwa (Vimechukuliwa badala ya) kwa neno moja la (kivumishi) adverb tulilolitumia katika mifano mwanzoni mwa pattern hii. mafungu haya ya maneno haya ni lazima yajibu swali "Where".

  Prepared by Muhseen bin Rajab Husayn (canoksan)

Sunday, August 04, 2002