Dictionary  home Qur'aan Islamic studies  home English main page sentences pattern 

  Muhraja's après ski & nocturnal English Language Program center

              sentence pattern three.

  Angalia katika sentensi hizi zifuatazo:

   The boy in the blue hat looked very happy.

  Kama ambavyo tulikwisha ona, maneno ambayo yameandikwa ki italic hutupa mifano ya patterns husika, hapa tunaona maneno hayo yametupa mifano halisi ya pattern three. ni muhimu kila tunaposogea katika pattern nyingine tujue tofauti kati ya pattern tuliyokwisha isoma na inayofuatia, haya yote tunaweza kuyajua kutokana na miundo au muundo wa maneno yaliyotumika katika pattern husika. Mfano katika pattern hii maneno yaliyoandikwa kwa italic hapo juu ni haya yafuatayo;

                                  Boy looked happy.

      Tuna noun (jina), adjective (kivumishi) na verb (Kitenzi), lakini pia twaweza kutumia verbs chache tu katika sentence pattern hii. Twaweza kuziita verbs hizi "linking verbs" (Verbs zinazohusiana) kwa kuwa huungana pamoja kwa karibu katika maneno yanayohusiana. Katika mfano hapo juu, Looked hufungamanisha boy na neno  happy.

      Hapa tunapata mifano zaidi ya sentence pattern three: Zinaonyesha (linking verbs) vitenzi vyenye mahusiano ambavyo hutumika sana;

     (The) yam tastes excellent.

    I remain faithfully. 

    Abdul looked miserable. 

    You appeared tired.

    It seemed new.

    Her dream rang true.

   The man became untreatable.

   Hassan grew old.

  The lunch smelt delicious.

  The mango feel unripe. 

She appeared very happy at the new

   Waweza ukatumia kifungu cha maneno badala ya kutumia adjective moja katika pattern hii. Kwa mfano;

     (The) ring looked of little value.

     (The) incident seemed of no importance.

         Haya ni mafungu ya maneno yenye tabia kama ya adjectives katika pattern hii, na hutumika sana sana baada ya verbs "Seemed, look, na appear" ingawa hazijitokezi mara kwa mara kama zifanyavyo katika vifungu vya maneno yanayo chukua nafasi ya adverbs katika sentences pattern two. 

    Matumizi ya linking verbs kwenye sentence patterns nyingine.

  Usishangae ukiona kuwa baadhi ya linking verbs hizi hutumika katika sentence patterns nyingine. Mfano;

(The) plant grew (quickly)        Sentence pattern one

(The) dog grew fat.                 Sentence pattern three.

   Hapa hakuna ugumu wowote katika kutofautisha na kutambulisha sentensi hizi mbili ndani ya sentence pattern sahihi ikiwa neno linalofuatia linking verbs ni  adjective kama vile "fat". Ingekuwa mfano wa sentence pattern One ikiwa neno baada ya verb lilikuwa adverb kama quickly.

   Hata hivyo, ugumu waweza tokea wakati neno likiwa linatumika lingeweza kuwa adjective au adverb, kama ilivyo hapa chini,

     The student appeared last

     The teacher looked hard

     Hata hivyo, unatakiwa uweze kujua na kutofautisha kutoka kwenye maelezo ambayo sentensi za namna hii huweza kuwa zimetokea, Uwe una adjective au adverb, au uwe huna, kwa hivyo, utajua kutokana na hayo mfano wa sentence pattern three au one

  By Muhseen Bin rajab Husayn (canoksan)

  04 August, 2002