Canoksanhilal Free Online Swahili English course

Sentences pattern 6

 Angalia katika sentensi zifuatazo.

             The man in the red car is a member of parliament.

      Maneno katika italic hutupa mifano ya pattern six.

            Man is a member of parliament.

  Tofauti pekee iliyopo kati ya sentensi hii na sentence pattern five ni verb hiyo. Katika sentence pattern six, twatumia verb "to be". Hapa kuna mifano michache,

   This is (the only Swahili English website.)

   It was (my first time I had eaten ugali)

   "English without tears" is my favorite English book.

    (That) car (there) is my friend's

          Waweza ukawa unashangaa sasa hivi kwa nini tumegawanya sentensi na kuzitenganisha na kuziweka katika patterns tofauti tofauti sentence pattern zenye kutumia verb be kutoka katika pattern zenye kufanana ambazo zinatumia linking verbs. Moja kati ya sababu ni kuwa "verb be" ni muhimu na ni mahsuus, ni maalum katika lugha ya Kiingereza. InshaaAllah, sababu nyingine itajulikana wakati tutakapokuja kuangalia namna gani sentence pattern zetu za kimsingi huweza kubadilishwa, kwa wakati huu unatakiwa usome tu na kutambua sentence pattern za msingi (ambazo ndio tunaendelea kuzisoma)

  Hadi hapa Inshaallah tuonane katika somo lijalo.

    By Muhseen bin Rajab Husayn (canoksan)

    05/08/2002