Canoksanhilal Free Online Swahili English course

Sentences pattern 7

 Angalia katika sentensi zifuatazo.

        The teacher in the white suit, who at the first time was teaching us in our new class room, picked up my pen when I lost it at the playing ground.

  Maneno katika italic hutupa mfano kamili wa sentence pattern seven:

      Teacher picked pen.

            Kama ilivyokuwa katika sentence pattern five na six, tuna verb inayosimama kati ya nouns mbili (majina mawili); lakini katika sehemu hii verb  hiyo sio "be" wala moja ya "linking verbs". Kuna mamia ya verbs tunazoweza kuzitumia katika pattern seven (hii tunayoendelea kuisoma sasa). Hii ni mifano ya sentence pattern seven:

     We told (them the) story.

     He denies (to let) me (in his sitting room)

     He explained (the) question.

    He tells (the) truth.

   (The) man tried your the shoes.

        Ubainisho wa noun inayofuatia verb.

   Unatakiwa ujue utambue tofauti kati ya noun inayofuatia verbs katika sentence pattern five na six, na zile ambazo huja baada ya ya verb katika sentence pattern seven. Katika pattern five na six, hizi nouns hurejea kwa mtu huyo huyo au kitu hicho hicho kama noun ambazo ni subjects na huwa baada ya verbs. Tazama mifano ifuatayo hapo chini;

    He became (a) technician.    (Hii ni pattern five)

   (The) man is (a) teacher.        (Pattern six).

       Katika sentence pattern seven, ilivyo, Noun ambayo hufuatia verb hurejea mtu tofauti au kitu tofauti kwenye noun ambayo huwa kabla ya verb,  Hebu tazama haya katika mifano ifuatayo ambayo tunayo, sheria hiyo itatumika isipokuwa wakati pronouns kama myself, himself, n.k zikitumika katika pattern hii:

   She braced herself.

   Don't put yourself in trouble.

   He shot himself.

    Verbs zitumikazo zaidi ya sentence pattern moja: 

Tumekwisha ona katika pattern three kuwa baadhi ya verbs zaweza kutumika katika sentence pattern zaidi ya moja. Hii hutokea hususan katika verbs nyingi ambazo hutumika katika sentence pattern One na Seven. Tazama mifano hii hapa chini;

 (a) (The) cigarrete burned (a) hole (in my pocket)                    

(b) (The) fire burned  (fiercely)   

     Kwaweza kuwa na ugumu kidogo katika  kuelewa au kubainisha kuwa (a) ni mfano wa sentence pattern Seven na (b) ni mfano wa sentence pattern one

II. Linking verb yaweza kujitokeza katika patterns tatu. Katika pattern three tulifananisha. Mifano kama hiyo ni kama 

 (The) dog grew fat (Sentence Pattern three)

(The) plant grew quickly (Sentence pattern one). Sasa tunaongeza :

     He grew vegetables.   (Sentence pattern seven)                                                                                       By Muhsin Bin Rajab Husayn (Canoksan)