allah-names.gif

allah-names.gif

Canoksanhilal-Qur'aan huwaokoa watu na hutuliza nyoyo zao, risala ya Allah kwa watu wote.
Make your own free website on Tripod.com

  Kwa jina la Allah mwingi wa rehma mwenye kurehemu.

Welcome to the noble recitation Qur'aan page direcories

CANOKSANHILAL ONLINE QUR'AAN DIRECTORIES PAGE.

 Canoksanhilal inawarahisishia wasomaji wake na wapenzi wa site hii wanaopenda Qur'aan kuisikiliza na kuisoma na kuihifadhi kwa kupitia site hii, Sikiliza Qur'aan kutoka kwa wasomaji (Dr.Ali bin Khudhayf, Sh.Abdul Baset, Sh.Menshawi na Khosari)

Kinachotakiwa katika computer yako ili uweze kusikia na kuendesha program hii ni 'software' zifuatazo

1. Flash player toleo la sita au juu ya hapo (Version 6.o),

2. Hardware ambazo ni speaker na sound cards.

    Kama huna flash, Click hapa uipate macromedia flash player

   Mambo ya kuzingatia unayotakiwa kujua kabla ya kuclick hapo;

    (a) Baada ya ku-Click utaona chini kidogo ya ukurasa utakaofunguka maneno, kwenye maneno haya 

           "INSTALL NOW " Click juu yake na muda mfupi tu, neno hilo liko kama hivi katika picha

install.gif

              flash   player itaingia kwa njia ya internet kwenye computer yako..

     (b) Kutegemeana na security setting yako uliyoifanya kwenye 

           computer yako, unaweza ukaona security warning box (yaani sanduku 

           la onyo la usalama wa computer yako ambalo kwa juu limeandikwa

          "Security warning kama ambavyo unaweza kuiona hapo kuliani mwako kwenye picha "

security.gif

"Yes" ili kuzikubali na kuziruhusu active x control 

     (c) Ukiona kijipicha cha macromedia Flash 6.0 na maandishi halafu 

        ukipitisha "Mshale unaoongozwa na mouse" juu yake unasikia sauti 

        fulani ujue tayari umesha maliza kuingiza macromedia flash player.

        Click hapa ili uanze kusikiliza tayari,

      Mambo ya kuzingatia katika kupata unachokihitaji kwa wale ambao hawajui lugha ya Kiingereza

     1. Bonyeza (Click) kwenye maandishi "RECITER 2.0"

         Subiri kidogo hadi imalize kuingiza data za kuendeshea Program, inaweza kuchukua sekunde chache au nyingi kutegemeana na server yako unayoitumia, (Utaona kwenye screen yako inakuwa nyeupe na kisha katikati kutakuwa na progress indicator ikijaza data kutoka angani ikikuhesabia kuanzia asilimia moja hadi mia moja, hapo itakufungulia Suuratul faatiha na utaiona kwenye screen,

   Kwenye maandishi ya kukuongoza yaliyopo kuliani mwako, mstari wa tano kutoka juu, utaona neno "faateha" basi click juu yake ili kuchagua sura ingine unayoitaka, Reciter itafungua orodha ya sura zote za Qur'aan ili uchague unataka ipi. click ile unayoitaka, hapo iachie reciter nafasi ili iweze kuichukua sura unayoitaka kutoka kwenye mtandao na iisafirishe kwa njia rahisi kwenye computer yako, utaona kuliani mwako progress indicator ikikuonyesha namna inavyochukua data kuanzia asilimia moja hadi mia moja, hizi data huhamishwa muda mfupi kutegemeana na "server" yako.

  2.    IKIWA UNATAKA MSOMAJI MMOJAWAPO KATIKA HAO WANAOHUSIKA

     Inawezekana ukahitaji asikusomee Abdul Baset na ukahitaji msomaji mwingine,samahani kuwa sasa hivi (Katika kipindi hiki kutokana na matatiz yasiyozuilika tunaye msomaji mmoja tu na hata hivyo mengi katika haya tuliyoyaeleza namna ya kufanya yamebadilika, msomaji wetu ni Menshaawi)

  Juu kabisa kwenye maelezo kuliani mwako, Click kwenye kimshale kilichopo kuliani mwa kisanduku kinachoelekea chini ili kukifungua.

   Utaona neno "option" ambalo lipo chini kabisa baada ya kufunguka kisanduku hicho click hapo.

  Hapo utaona orodha ya wasomaji wetu, Chagua mmoja unayemtaka akusomee kwa kuclick kwenye alama ya kiduara cheupe kilichopo kushotoni mwa jina la msomaji.

 Click tena kwenye neno "Option" hapo juu kabisa ili kufungua kisanduku chako hicho na utaona kwenye neno la pili kwenye orodha limeandikwa "reading & repetition" Click hapo ili uanze kusikiliza na huku unayaona maadishi ya sura unayoitaka kwenye screen yako

  3. Ikiwa wewe unahitaji sehemu ya sura

           Labda kutoka aya fulani hadi aya fulani unataka kuihifadhi yabidi uclick kwenye mishale iliyopo kwenye mstari wa kwanza wa maadishi "From verse" ili uchague namba ya aya unayotaka kuanzia na kisha utaclick kwenye mishale ya neno la mstari wa tatu lililoandikwa "to verse" ili kuchagua namba ya aya unayotaka kuishia.

  Neno "Verse repetition" hutegemeana na aya unavyotaka kila aya ijirudie mara ngapi (Yaani msomaji asome kila aya mara ngapi kabla ya kusoma aya inayofuatia ili wewe katika kurudiwa rudiwa huko uweze kuhifadhi.

  Katika neno "All verses" hapa unachagua kwamba kuanzia aya uliyoichagua kuanza nayo hadi ile uliyoichagua kuishia nayo zirudiwe mara ngapi (Kuanzia mwanzo hado mwisho)

  Kuna vitu vingine kama "Muda wa kusimama iwe sekunde ngapi kati ya aya hadi aya inayofuatia ili uweze kufuatiliza kama unataka kufuatishia kisomo hiki.

  Katika kuanza kusikiliza, Click kwenye kimshale chini kuliani upande wa mkono wa kulia ambacho kimshale hicho kimeelekea kulia, ukitaka kuisimamisha kwa muda ili baadaye uendelee na kisomo baada ya dakika chache, utahitajika kuckick kwenye vimstari viwili vilivyopo upande wa kulia wa mshale huo (Ulioelekea kulia) na ukitaka kuisimamisha utaclick kwenye kisanduku kilichopo kushotoni kabisa chini ya recitor (Upande wa kushoto wa vimstari viwili)

  Na hadi hapo tunakutakia usikilizaji mwema wa Qur'aan tukufu,

      Ukitaka site nyingine za kusikilizia Qur'aan tukufu kutoka katika maelekezo ya canoksanhilal Click hapa

Tuma maoni yako na changia mawazo katika kuendeleza elimu ya Kiislamu kwenye mtandao. Anuani zetu ni canoksan@yahoo.com 
au hilalshukri@yahoo.com

  By Muhseen bin Rajab Husayn

Sunday, July 21, 2002