Muhraja's après ski& nocturnal English language program course centre
Katika lugha ya Kiingereza tuanza kutaja matunda yale ambayo yanapatikana katika mazingira ya hapa Afrika na majirani wake:
Kutokana na kushindwa kujua majina mengine ya matunda hayo kwa Lugha ya Kiswahili, nimeweka picha yake ili msomaji atakapo click katika jina itokee picha ya tunda hilo lililotajwa, hii ni katika jitihada za kurahisisha usomeshaji. Naomba sana kwa msomaji yeyote anayefahamu matunda yaliyokosekana majina yake hapa awasiliane na mimi kwa anuani iliyotajwa chini ya ukurasa mkuu.
Naomba sana ushirikiano wenu katika kuendeleza "website" hii ya Kiswahili kwa kusomeshea Kiingereza. Vilevile kwa matunda ambayo hatuyataja hapa ambayo unajua Kiswahili chake, waweza kututumia kwa kutumia anuani yetu iliyotajwa.
Tunapenda sana kupokea e mail zenu.
Click (bonyeza kwa kutumia "mouse" yako upande wako wa kushoto neno lililo na alama nyeupe ili uone picha ya jina hilo.
JINA MAANA MATAMSHI
A mango embe mengo.
A guava pera gwave
A papaya/ a pawpaw papai (papaya/popo)
A cashew apple bibo. (Keshiu epo)
A custard apple tope tope (kastad epo)
An avocado or ("avokado" au " eligeta epo")
( alligator apple) parachichi
A melon tikiti maji. (melon)
An orange chungwa. (orenj )
A tangerine chenza. (tenjirin)
A baobab fruit ubuyu.
A tamarind ukwaju.
A date tende.
An apple epo.
A strawberry (tunda nyanya/ (jamii ya tunda damu) tazama picha hapo juu)
A jackfruit fenesi.
Currant zabibu kavu ndogo.
A banana ndizi.
A jujube fruit tunda la mkunazi.
An olive Zeituni.
An apricot mishmish.
A peach fyuliks, (wengine huita fyoks)
A pear peaz
A grapefruit balungi/dalansi.
A damson Zambarau.
A lime ndimu.
A breadfruit shokishoki.
A plum tunda kama zambarao vile lilivyo.
grapes zabibu.
A nutmeg kungumanga.
A pomegranate komamanga.
Mulberry forosadi
Cucumber tango.
A pineapple nanasi.
Sour sop stafeli, tomoko.
Sweetsop topetope, angalia custard apple hapo juu.
A passion pasheni.
Pitaya /pitahaya/ (or dragon fruit) tunda fulani laini na lenye sura tofauti na tuliyoyazoea.
Gherkin aina ya tango dogo.
Other fruits are (matunda mengine ni:)
Citrus matunda jamii ya machungwa.
Durian duriani.
Grumichama matunda fulani ambayo ni makubwa kama chungwa na yaivapo huwa na rangi ya maji ya
machungwa.
Macadamia nut matunda yanayofanana na mapera kwa umbo na ukubwa.
Wampi matunda yafananayo na pashen bivu kwa rangi.
Sapodillas aina fulani ya matunda yenye umbo la bilinganya (Umbo la balbu)
Pippin aina fulani ya apple.
Prune plum kavu.