Muhraja's après' ski & Nocturnal English program
Make your own free website on Tripod.com

 

                                                                          

        MUHRAJA'S ENGLISH PROGRAM

KaribuCANOKSAN AND HILAL HOME PAGE

  Home; Greetings; nouns; pronouns; verbs; adjectives; adverbs; Tenses;

    Kusoma lugha ya Kigeni ni bahati kubwa sana, ni sawasawa na kusafiri nchi ya kigeni, Ni jambo la bahati sana na ni zuri, lakini wakati mwingine linachosha sana,  Kwa mwanafunzi ambaye yupo makini na somo hili na ana nia kweli ya kusoma, nimeandika mambo muhimu ambayo yatamsaidia kuweza kuanza kozi yake ya Kiingereza na pia kupata kuweka msingi wa kujua lugha. Website  ambayo inakuletea somo hili katika lugha yako ya Kiswahili, imeasisiwa  na "Muhraja's  après ski and Nocturnal English Program" iliyopo mtaa wa Yombo Temeke Chang'ombe inayofundisha tuishen ya kiingereza kila  na usiku kuanzia saa moja hadi saa tatu jioni.

               Madhumuni makubwa ya home page hii ni kukuza uwezo wa kupata msamiati na mambo mengine muhimu kwa mwanafunzi anayeanza kujifunza Kiingereza,  Kwa wanafunzi ambao wanajua Kiswahili lakini hawajui Kiingereza natumaini sasa watapata wepesi kiasi fulani kujisomea na kujifunza Lugha hii ya Kiingereza kwa kutumia homepage hii.  Malengo maalum yaliyomo ni katika kumsaidia mwanafunzi anayetumia Lugha ya Kiswahili katika kujifunza lugha ya Kiingereza na pia anaye tumia lugha ya Kiingereza katika kujifunza Kiswahili, Amma hii "website" itamsaidia pia  mwanafunzi  aweze kuelewa masomo yake vizuri shuleni kwa kuwa Kiingereza ndicho kinapotumika katika masomo yote hasa Tanzania na Afrika ya mashariki. Katika homepage hii yapo majina ya vitu ambayo nimeona ni bora kuyawekea picha katika kuyaeleza kutokana na kushindwa kuyaweka bayana katika lugha ya Kiswahili, kwa kuwa dhumuni langu ni kueleweka basi si vibaya nikitumia picha (taswira hizo) pale nitakapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.Naomba sana watembeleaji wa "website" hii watumie nafasi hii katika kuisoma na kuielewa na kutoa mawazo yao katika kuiendeleza ili iweze kutoa huduma ya hali ya juu kuliko ilivyo sasa.

              Kutokana na matatizo yanayo wakabili  wanafunzi katika kujifunza  Lugha ya Kiingereza ambayo nimeyakuta wakati wa kuwasomesha, nitajaribu kuyaweka wazi tu baadhi ya kwa muhtasar, lakini kwanza kabisa nieleweke kuwa hii "site" sio ya wanafunzi wa shule peke yao, kwa hiyo nitaanza kuandika mambo muhimu hata kwa yule ambaye ndio anaanza kujifunza mwenyewe aweze kufaidika.

         Amma kwa yule anayetaka ajue harakaharaka salamu na mambo mengine madogo tunaanza moja kwa moja na somo letu hilo bila kupoteza wakati. Click hapa.  Kwa kawaida tunajua kuwa kila lugha ina  fasaha yake, na lafidh yake.

                       Kila Lugha ina majina, (nouns). Twaweza kuwa tunahitaji kujua majina ya vitu Click hapa

                   Tunavyo viwakilishi (pronouns) yaani maneno yanayo simama badala ya majina. mfano badala ya kumtaja mtu aliyekwisha au kitu, mahali n.k palipokwisha julikana aupalipokwisha tajwa mwanzoni, badala yake utasema, "yeye' au "sisi" 'wao', hapo, ile  n.k. Kama malengo yako ni kusoma hizo, click hapa uingie moja kwa moja darasani

Viwakilishi ni muhimu sana katika kila Lugha, navyo viko aina mbali mbali. Tunazo verbs (yaani vitenzi/vitendo), pia kuna maneno muhimu sana ambayo yanatumika mara kwa mara katika lugha hii, nimejaribu kuyabainisha na InshaaAlah hivi karibuni mtayaona hewani,

   Pamoja na hayo yote, katika jitihada za kuifundisha lugha hii kwa njia rahisi kwenye internet, nimeazimia kuweka somo maalum la namna ya kutumia verbs kwa kuzitambulisha katika makundi mbali mbali kwa mujibu wa kanuni za verbs hizo,somo hilo huitwa (verbs patterns). Siyo hivyo tu, bali hata kanuni za kuunda sentensi ambazo zipo katika somo lijulikanalo kama "sentences patterns". Yapo vile vile maneno yanayo changanya watu ambayo tumejaribu kuyaweka wazi. (muda wowote inshaaAllah yatakuwa angani)

    Tunakuomba ndugu msomaji utoe maoni yako juu ya website hii ambayo bado ipo katika kuendelezwa, toa maoni yako, ikosoe, tuma e mail katika anuani yangu canoksan@yahoo.com  au hilalshukri@yahoo.com na waweza pia kunipa maana fupi ya baadhi ya maneno ambayo nimeshindwa kuyajua kiswahili chake.

 

               To  Return back to the top click here

 

Click hapa ikiwa unataka Kamusi ya Kiswahili kwa Kiingereza au Kiingereza kwa Kiswahili